Wakazi wa Kinondoni Mahakamani
wamelalakia maji yaliyozingira nyumba zao kutokana na baadhi ya wakazi hao
kujenga katika mkondo wa maji.
Akizungumza leo mkazi wa
eneo Bi. Khadija Hamis amesema kutokana na mvua za masika zinazoendelea
kunyesha wanapata adha ya maji hayo yanayotuama kwenye eneo hilo.
Amesema kuwa baadhi ya
wakazi wa eneo hilo wamezingirwa na maji kwa wiki mbili na hakuna chochote
kinachofanyika.
Aidha amesema kutokana na
hali hii kuendelea wanaiomba serikali kutatua tatizo hili mara baada ya kuisha
masika.
Mvua zinazoendelea kunyesha
maeneo mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam iliyoanza kunyesha wiki
iliyopita, zimesababisha maafa, uharibifu wa miundombinu ya baarabara pamoja na
baadhi nyumba katika eneo la Kinondoni Mahakamani kuzungukwa na maji ya mvua jijini
Dar es Salaam.
Mwanafunzi akikwepa dimbwi la maji machafu ya mvua
kama yanavyoonekana pichani leo jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo, mvua hizi
zinazoendelea zimeendelea kuleta maafa na athari kubwa maeneo ya Ubungo
Kisiwani nyuma ya hoteli maarufu ya Land Mark. Baadhi ya wakazi wa eneo hilo
wamekosa makazi kwa kubomokewa na nyumba zao na kuomba serikali iwasaidie
kutokana na hali iliyowakuta.
Akiongea na Wor’Out Media
Blog, Mjumbe wa Mtaa wa Hekima Kata ya Ubungo Kisiwani Bondeni, Bi Tabu
Selemani, anashangazwa na hali ilivyojitokeza kwa mvua hizi, kwani mara nyingi
mafuriko huwa yanawatesa watu wa mabondeni tofauti na mvua hizi.
“Mvua hizi zimeathiri
sana nyumba zilizokuwa hazihisiwi kupata athari za mvua kwamiaka yote.”
Maji yatamalaki kwenye viunga vya Mtaa wa Hekima, Ubungo Darajani
Maji yatamalaki kwenye viunga vya Mtaa wa Hekima, Ubungo Darajani
Maji yatamalaki kwenye viunga vya Mtaa wa Hekima, Ubungo Darajani
Maji yatamalaki kwenye viunga vya Mtaa wa Hekima, Ubungo Darajani
Maji yatamalaki kwenye viunga vya Mtaa wa Hekima, Ubungo Darajani nyumbani kwa Mjumbe wa Mtaa huo.
Tazama tofali za nyumba zilizo athiriwa na mafuriko hayo
Mitaa yote imeathiriwa na kujaa matope baada ya maji yaliyojaa kwenye viunga vya makazi ya waishio bondeni kupungua
No comments:
Post a Comment