BAADA ya kusimama kwa kipindi cha takribani wiki tatu Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena Jumamosi Mei 6 na Jumapili Mei 7,
mwaka huu kwa jumla ya michezo sita.
Kwa mujibu wa ratiba, michezo ya Jumamosi kutakuwa na michezo mitano
ilihali Jumapili kutakuwa na mechi moja.
Afisa habari wa Shiriukisho la Mpira wa Miguu Alfred Luacs amesema kuwa
michezo ya Jumamosi itakuwa ni kati ya Toto African na JKT Ruvu katika Uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa
Mwadui kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Kagera Sugar itaalikwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini
ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Young Africans ya Dar es Salaam itaialika
Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Siku hiyo ya Jumamosi Mei 6, mwaka huu Azam FC itaialika Mbao FC ya
Mwanza kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Mbagala, Dar es Salaam ilihali
Jumapili kutakuwa na mchezo kati ya Simba SC na African Lyon kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Wakati mechi zote zitaanza saa 10.00 jioni, mchezo kati ya Azam na Mbao
utaanza saa 1.00 usiku.
No comments:
Post a Comment