Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena
Saidi akifungua maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani
kimkoa yaliyofanyika kwenye ukumbi wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Tanga
(Tanga Press Club), kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari
Mkoani Tanga, Hassan Hashim kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi
wa Habari Mkoani Tanga, Lulu George
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani
Tanga, Hassan Hashim akizungumza katika maadhimisho hayo.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari
Mkoani Tanga, Lulu George akizungumza katika maadhimisho hayo kushoto ni Katibu
Msaidizi Alex Abraham
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari
Mkoani Tanga, Hassan Hashim kushoto akifurahia jambo na Katibu Tawala wa Mkoa
wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi mara baada ya kupokea cheti cha kuripoti habari
za majanga na hali hatarishi, mafunzo waliyoyapata mkoani Morogoro hivi
karibuni
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari
Mkoani Tanga, Lulu George naye akipokea cheti hicho kushoto ni Kamanda wa
Polisi Mkoani Tanga, Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benedict Wakulyamba
kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga, Hassan Hashim
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Waandishi
wa Habari Mkoani Tanga, Amina Omari naye akipokea cheti hicho
Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa Habari na Mwandishi
wa Clous TV Mkoani Tanga Zawadi Kika naye akipokea cheti
Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa Habari na
mwandishi wa gazeti la Citizen Paskal Mbunga naye akipokea cheti.
Mmiliki wa Blog ya Tanga Kumekucha na Mwanachama
wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Tanga, Salum Mohamed naye akipokea cheti
hicho
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri
wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorah Killo akizungumza jambo kwenye
maadhimisho hayo
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benedict Wakulyamba akizungumza jambo kwenye
maadhimisho hayo
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani
Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ili
kuweza kunufaika na fursa zinazopatikana kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tanga
Press Klabu, Lulu George
Afisa Uchunguzi kutoka Takukuru Mkoani Tanga, Frank
Mapunda akisisitiza jambo kwenye maadhimisho hayo leo
Afisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani
Tanga (NHIF) Sophia akisisitiza jambo kwenye maadhimisho hayo kulia ni Meneja
wa Mfuko huo Mkoani Tanga, Ally Mwakababu anayefuatia ni Makamu Mwenyekiti wa
Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga (Tanga Press Club) Lulu George
Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga
wakiwemo wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa ziki wakilishwa
kwenye maadhimisho hayo
Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga
wakiwemo wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa ziki
wakilishwa kwenye maadhimisho hayo
Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakiwemo wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa ziki wakilishwa kwenye maadhimisho hayo
Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakiwemo wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa ziki wakilishwa kwenye maadhimisho hayo
Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakiwemo wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa ziki wakilishwa kwenye maadhimisho hayo
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani
Tanga (NHIF), Ally Mwakababu kulia akiteta jambo na Mwandishi wa gazeti la
Mtanzania katikati Amina Omari kushoto ni Ofisa wa Mfuko huo mkoani Tanga
Sophia
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani
Tanga (Tanga Press Klabu) Neema Omary kulia na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Klabu hiyo, Amina Omari wakifuatilia matukio mbalimbai
KATIBU Tawala Mkoa Tanga
Mhandisi Zena Said ameziagiza taasisi za Serikali na mashirika ya umma kutoa
ushirikiano kwa waandishi wa habari pindi wanapohitaji taarifa kutoka kwenye
taasisi hizo kwa ajili ya kuhabarisha umma.
Ameyazungumza hayo leo
wakati wa kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani ambapo Mkoa
Tanga maazimisho hayo yalifanyika katika ukumbi wa klabu ya waandishi wa habari
na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na zisizo za
kiserikali.
Hatua hiyo imekuja mara
baada ya waandishi wa habari kutoa malalamiko yao mbele ya Katibu Tawala huyo
wa Mkoa ambae alikua mgeni rasmi katika maazimisho hayo ya kuwa zipo baadhi ya
taasisi za Serikali kushindwa kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari pindi
wanapohitaji kutekeleza majuku yao ya kazi.
Burhan Yakubu ambae ni
mjumbe na mwaandishi wa habari alisema kumekuwepo na utaratibu usioendana na
maadili ya kiuwandishi katika Hospitali kuu ya Rufaa ya Bombo kwa kutengeneza
urasimu wa kupatikana kibali kutoka kwa katibu tawala Mkoa wakati mwandishi
anapohitaji kupatiwa tariifa zozote kutoka katika Hospitali hiyo.
“Tumekuwa tukikwama
kutekeleza wajibu wetu hasa tunapohitaji kupata taarifa katika Kuu ya Rufaa ya
Bombo na kulazimishwa mpaka tupate kibali kutoka kwa katibu Tawala jambo ambalo
limekuwa liktkwamisha katika shughuli zetu”Alisema Yakubu.
Akitolea ufafanuzi
malalamiko hayo Mhandisi Zena alisema taasisi zote zinapaswa kutambua kuwa
wanahabari wanahaki ya kupatiwa taarifa sahihi kwa lengo la kuihabarisha jamii
na hakuna sababu za kuweka vikwazo kwao kwa lengo la kuwakwamisha kutimiza
majukumu yao.
Mhandisi Zena alisema
zimekuwepo taarifa za malalamiko kwa waandishi kuwa zipo baadhi ya tasisi kama
Hospitali ya Rufaa ya Bombo kutokutoa ushirikiano wa kutosha kwa waandishi wa
habari pindi wanapotaka kutekeleza wajibu wao kwa manufaa ya wananchi na Taifa
kwa ujumla.
“Tusiwawekee mipaka
waandishi wakati wanapotaka kutekeleza majuku yao na tayari nimekwisha toa
agizo sio Hospitali ya Bombo tu hili ni kwa taasisi zote,hakuna jambo
linaloweza kufanyika na mwananchi akaweza kulipata kwa wakati ikiwa hakuna
waandishi,tunatambua umuhimu wenu na thamani yenu ni kubwa kwa Taifa
Hili.”Alisema
Hata hivyo alitumia fursa
hiyo kuwaomba waandishi wa habari kutumia kalamu zao vema na kuwepo na maadili
yatakayokuwa na maslahi mapana kwa ajili ya amani ya nchi na kujiepusha na
taarifa zitakazoweza kuliingiza Taifa kwenye machafuko.
Katika hatua nyingine
Mwandishi wa Tanzania Daima Mkoani Tanga Mbaruku Yusuph alitaka kupatiwa
ufafanuzi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa Tanga, Kamishna Msaidizi, Mwandamizi
wa Polisi Benedict Wakulyamba, juu ya usalama wa waandishi wa habari
wanapotekeleza wajibu wao hasa katika mikutano ya kisiasa.
Mbaruku alisema hivi
karibuni kumeripotiwa kutokea matukio kwa baadhi ya waandishi wa habari maeneo
mbalimbali hapa nchini kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kushindwa
kuwajibika katika harakati zao za kupata habari kwa lengo la kuhabarisha umma
na kujenga hofu kubwa kwa baadhi yao juu ya usala wa maisha yao.
Kamanda wakulya alisema
jukumu la usalama lipo mikononi mwa jeshi hilo na wajibu wa polisi kutambua
uwepo wa waandishi na umuhimu wao katika kila tukio ambapo alitoa rai kwa
waandishi hao kuziona dalili za uvunjifu wa amani na kuanza kujiepusha mapema
kabla ya madhara makubwa hayaja tokea.
No comments:
Post a Comment