Waziri wa Mambo ya Nje wa
Palestina Dr. Riyad Maliki, Jumanne ya wiki hii amekaribisha matokeo ya kura ya
Bodi ya Utendaji ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO),kwa kupitisha maazimio mawili yanayohusu
Palestina,ambayo ni: Palestina inayokaliwa kimabavu na Taasisi za kiutamadui na
kielimu. Nchi zipatazo ishirini (20) zimepitisha maazimio hayo, huku nyingine
kumi (10) zikipinga na ishirini na tatu (23) hazikupiga kura.
Katika taarifa yake kwa
vyombo vya habari, Maliki amezishukuru nchi hizo zilizopitisha maazimio hayo
mawili na kujua wajibu wake katika kuhifadhi maeneo matakatifu nchini
Palestina. Alisisitiza kuwa "licha ya jitihada zinazotolewa na serikali
kutokana na tamaa ya serikali ya Israeli katika kudhoofisha maazimio ya
Palestina ndani ya UNESCO, hata hivyo dunia imepitisha maazimio yetu kwa
kuchagua haki iko wapi mbele ya usawa, kazi na sera zake haramu .
Ameongeza kusema kwamba,
hilo limethibitisha kushindwa kwa kampeni nyingi za Israeli dhidi ya maazimio
yahusuyo Palestina, Jerusalemu na UNESCO, huku wakishindwa pia wale wote
waliounga mkono hatua ya kudhoofisha maazimio hayo, miongoni mwa nchi
mbalimbali, vikundi, taasisi na hata watu binafsi.
Amesema maazimio
yameonesha nyanja za kihistoria, kiutamaduni na urithi wa mji wa
Jerusalemu,jambo linalosisitiza umuhimu wa kupeleka mwakilishi wa kudumu wa
UNESCO mjini Jerusalemu,ili kufuatilia ukiukwaji na kuondoa vitendo vya
uharibifu vinavyofanywa na Israeli,ambayo inafanya juhudi kufuta urithi wa
kihistoria,kidini na wa kiutamaduni wa mji huo, hatimae kubadilisha kabisa
hadhi yake.
Waziri huyo wa Mambo ya
Nje wa Palestina, kwa upande mwingine ameelezea kutoridhika kwake na msimamo wa
nchi zilizokataa kupitisha maazimio hayo mawili,kwa mtazamo wa kushajihisha
kuendelea kwa utawala wa kivamizi na vitendo vyake haramu mjini Jerusalemu
inayokaliwa kwa mabavu. Pia kushuka kwa misimamo na misingi ya nchi hizi,
ambazo baadhi yake zinadai kutetea misingi ya sheria za kimataifa na haki za
binadamu.
Ametilia mkazo kwa
kusema, "Sisi tutaendelea kutetea urithi wetu, utamaduni wetu na uwepo
wetu, huku tukikabili kampeni zote za kuvuruga hilo na kuziharibu,
zinazoongozwa na mamlaka ya kivamizi ya Israeli. Vilevile mapambano ya silaha
kwa mujibu wa sheria za kimataifa na matakwa ya taifa la Palestina lenye uwezo
wa kujipangia mustakabali wake uliepukana na uvamizi”.
Aidha, ametoa wito kwa
mataifa yote duniani kubeba majukumu yao na si kuingilia kazi za UNESCO, wala
kuihamasisha Israeli kama ndio taifa la kivamizi kuendelea kufanya maovu yake.
Pia Ametoa wito kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa, hasa UNESCO, kuulinda urithi
wa Jerusalemu, utamaduni na historia yake, Jerusalemu ambayo ndio mji mkuu wa
Palestina, kutokana hatua zote za kuvuruga ustaarabu wa mji huo.
No comments:
Post a Comment