“MANENO ni mawili tu “KA
na TA” ukiunganisha Kata, asiyelipa kateni umeme” Hayo yalikuwa ni maneno ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, wakati
akitoa hotuba ya uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme
mkoani Mtwara miezi michche iliyopita.
Kufuatia maagizo hayo ya
Rais, Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa wake, Dkt. Tito Mwinuka, aliitisha mkutano na waandihi wa habari na
kutoa ilani kwa wadaiwa wote “sugu” wa bili za umeme kuwa walipe madeni yao
vinginevyo huduma ya umeme itasitishwa.
Baada ya tangazo hilo,
baadhi ya taasisi za serikali likiwemo Jesho la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania,
kupitia kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo, naye aliitisha mkutano na
wanahabari na kueleza kuwa JWTZ italipa sdeni lake na kuagiza wahusika wafanye
hivyo mara moja.
Leo hii Mei 4, 2017,
Meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali, aliwaita
waandishi wa habari ofisini kwake na kuwaeleza kuwa taasisi za umma na binafsi
zilizo katika mkoa wake, zilikuwa zikidaiwa jumla ya shilingi Bilioni 7, ambapo
taasisi za serikali pekee zilikuwa na deni la shilingi bilioni 6 na kwa
sasa tayari zimelipa jumla ya shilingi bilioni 2 na kubaki deni la shilingi
bikioni 4.
“Hizi taasisi za umma
tumeingia nazo mkataba na kwakweli wameanza kulipa na tunaendelea kuwahimiza
wafanye hivyo ili wasije kukosa huduma ya umeme.” Alisema Mhandisi Nangali.
Aidha alisema taasisi
binafsi zinadaiwa shilingi Bilioni 1 na nyingi kati ya hizo hazijaingia mkataba
wa malipo ya madeni yake na TANESCO kwa hivyo akatahadharisha kuwa TANESCO
haitasita kuchukua hatua za kusitisha huduma ya umeme na kwa kuonyesha kuwa
Shirika halifanyi mzaha, leo hii kampuni mbili moja ikimilikiwa na
mfanyabiashara maarufu Fida Hussein iliyoko Vingunguti wilayani humo imesitishiwa
huduma ya umeme kufuatia deni la shilingi Milioni 29.
Kampuni nyingine
iliyoonja joto ya jiwe ni Iprint iliyoko eneo la Banda la Ngozi
kandokando ya barabara ya Nyerere, kampuni hiyo hadi kufikia leo Mei 4, 2017
ilikuwa ikidaiwa jumla ya shilingi Milioni 16,95.
Maafisa wa TANESCO
waliokuwa kwenye operesheni ya “kukata” umeme kwa wadaiwa sugu, walikuwa na
stakabadhi zinazoonyesha kuwa kufikia leo Mei 4, 2017 kampuni hizo mbili
zikikuwa zikidaiwa madeni hayo.
Mhandisi wa kudhibiti mapato TANESCO mkoa wa
Ilala, Daniel Kimaro, akizungumza na waandishi baada ya kusitisha huduma ya
umeme kwenye kampuni ya Iprint.
Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO),
mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, wakiwa na kifaa cha kukatia umeme, tayari
kwa kazi kwenye transfoma ya kupeleka umeme kwenye eneo la kiwanda eneo la
Vingunguti
Mfanyakazi wa TANESCO kivaa gloves tayari kukata
umeme
Meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala jijini
Dar es Salaam, Mhandisi Athanasius Nangali (kulia), akiwa na Afisa kutoka idara
ya fedha TANESCO makao makuu, akizungumza na waandishi wa habari
Hii ni stakabadhi ya leo Mei 4, 2017
ikionyesha kampuni ya I print ikidaiwa shilinhi milioni 16.95
Baadhi ya wafanyakazi wa Iprint
wakitafakari baada ya huduma ya umeme kusitishwa
Maafisa wa TANESCO makao makuu,
wakimsikiliza meneja wa kiwanda cha Fida Hussein
Wanahabari wakiwa kazini
Mhandisi Athanasius Nangali (kulia),
akiongea na waandishi wa habari
No comments:
Post a Comment