Samatta aonesha ubabe wake Genk - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, May 28, 2017

Samatta aonesha ubabe wake Genk

Streika wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameonesha ubabeb usiku wa jana kwa kuifungia klabu yake bao moja pale timu hiyo iliposhinda  3-0 dhidi ya Sint-Truiden.
Mbwana Samatta

Bao hilo linakuwa bao lake la 20  katika mechi 59 tangu ajiunge na Genk Januari mwaka jana akitokea TP Mazembe ya DRC.

Kati ya mechi hizo 59, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 41 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 37 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 27 msimu huu.

Mechi 21 kati ya hizo alitokea benchi, 8 msimu uliopita na 13 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao hayo 19, 14 amefunga msimu huu na tano msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages