UCHAGUZI wa viongozi wa
Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu (TAFCA) Mkoa wa Kinondoni uliokuwa ufanyike
Mei 7 mwaka huu jijini Dar es Salaam sasa umesogezwa mbele hadi Juni 4.
Uamuzi wa kusogeza mbele
uchaguzi huo umetokana na mwitikio mdogo wa uchukuaji fomu kwa wagombea. Muda
wa uchukuaji fomu sasa umeongezwa hadi Mei 7 mwaka huu.
Fomu kwa ajili ya
wagombea zinatolewa kwenye ofisi za Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya
Kinondoni (KIFA) kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni.
Ada ya fomu kwa wagombea
wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi na
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TAFCA ni sh. 50,000 wakati Mhazini, Mhazini Msaidizi
na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni sh. 30,000.
Ajenda ya uchaguzi
itatanguliwa na Mkutano Mkuu wa Kawaida ambao mbali ya taarifa ya utendaji,
Kamati ya Utendaji inayomaliza muda wake pia itawasilisha ripoti ya mapato na
matumizi.
Kamati ya Uchaguzi ya
TAFCA Kinondoni inaongozwa na Mwenyekiti wa zamani wa TAFCA, Ramadhan
Mambosasa.
Kamati ya Utendaji ya
TAFCA Kinondoni inayomaliza muda wake inaongozwa na Mwenyekiti Eliutery Mholery
(0715 621 667) na Katibu Mkuu wake Mbwana Makata (0655 520 129).
No comments:
Post a Comment