Ni kazi inayohitaji
mhudumu atumie nguvu nyingi za mwili wake.
Sasa, watafiti
nchini Kenya wanasema kunaweza kuwa na changamoto nyingine kwamba wahudumu wa
bodaboda wanakabiliwa na hatari ya kupoteza uwezo wao wa uzazi.
Baada ya kufanya
utafiti, waligundua kwamba waendeshaji boda boda walikuwa katika hatari ya
kutoweza kutanua mishipa ya damu kwenye uume wakati wa kushiriki tendo la ngono.
Mmoja wa watafiti
hao Isaac Wamalwa ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta aliiambia
Wor’Out Media kwamba suluhu huenda likawa ni kutumiwa kwa kiti maalum ya
waendesha baiskeli ambayo hakitadhuru uume wa waendeshaji.
Bw Wamalwa ambaye ni
mtaalamu wa masuala ya afya ya uzazi alifanya utafiti miongoni mwa vijana eneo
la Bungoma, magharibi mwa Kenya.
Walichunguza
wahudumu 115 wa boda boda wa umri wa chini ya miaka 40 eneo hilo,
wakishirikiana na wataalamu wa afya ya uzazi kutoka Hospitali ya Taifa ya
Kenyatta na Chuo Kikuu cha Nairobi.
"Tuliwachunguza
vijana waendeshaji wa bodaboda Bungoma na matokeo yalikuwa ya kushangaza. Kwa
jumla, tuligundua kwamba zaidi ya theluthi moja ya waendeshaji bodaboda,
asilimia 35.9, ya washiriki walikuwa na matatizo ya kuweza kusimika,"
aliambia gazeti la Standard la Kenya.
Anasema tatizo lilitokana na kuendesha baiskeli hizo kwa muda
mrefu.
Bw Wamalwa anasema
wote walioendesha baiskeli kwa zaidi ya saa 60 kwa wiki, walikuwa na matatizo
ya kiafya.
Anatahadharisha pia
kwamba maelfu ya vijana wanaofanya mazoezi kwenye vituo vya mazoezi mijini, kwa
Kiingereza gym, ambapo huendesha baiskeli zisizosonga, wanakabiliwa na hatari
sawa na hiyo.
"Ujumbe wetu ni
muhimu kwao pia, kwamba wanafaa kuwa wanapumzika kwa muda kutoka kwa kazi yao.
Anasema wanapojikakamua kutafuta posho, wanafaa pia kujali uwezo wao
kitandani."
Wataalamu wengine sita kutoka Chuo Kikuu cha Moi walifanya
utafiti mjini Eldoret, magharibi mwa Kenya, na kupata matokeo yanayokaribiana
na ya Bw Wamalwa.
Waliwachunguza
wahudumu wa dbodaboda 131 wa umri wa kati ya miaka 18 na 65, umri wa kadiri
ukiwa miaka 40.
Waligundua kwamba
asilimia 76 kati yao walikuwa na matatizo kitandani.
Watafiti hao pia
walidokeza kwamba tatizo hilo huenda linatokana na kuendesha baiskeli kwa muda
mrefu.
No comments:
Post a Comment