Mgahawa wa Aiskrimu uliolipuliwa
Shambulio hilo
limetokea wakati wa jioni baada ya watu wakiwa wanaendelea kula futari, katika
kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani.
Eneo hilo linakaliwa
na watu wengi wa madhehebu ya Shia, huku habari zikisema kuwa ndio walikuwa
walengwa.
Kufuatia shambulio
hilo mjumbe wa Marekani katika kikosi cha Muungano wa majeshi yanayopambana na
kundi la Islamic State Brett McGurk amelaani shambulio hilo lililotokea jana
usiku.
Amesema shambulio
hilo lililofanywa na IS ni baya kutokana na kulenga watoto na familia zao ambao
walikuwa wakiburudika kwa kula aiskrimu wakati wa jioni baada ya mfungo wa
Ramadhan.
No comments:
Post a Comment