Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsimamisha kazi Ndugu Castory
Manase Nkuli Afisa Mipango Miji wa Lindi kuhusu tuhuma za kumilikisha ardhi
kinyume cha sheria.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kushoto) wakihakiki nyaraka na Mkuu wa
Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi (kulia) katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani
Lindi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey
Zambi, watendaji na viongozi wa Mkoa wa Lindi wakiwa katika mkutano wakati wa
ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango
Miji na Vijiji Bi. Imaculate Senje akizungumza kuhusu utaratibu za upangaji
miji na umilikishaji ardhi katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani
Lindi.
Ndugu Castory Manase Nkuli
Afisa Mipango Miji wa Lindi akijieleza kuhusu tuhuma zinazomkabili mbele ya
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na na Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikagua mafaili katika masijala ya
ardhi mkoani Lindi ambapo alibaini mapungufu ya kutokuwa na usahihi wa uwekaji
kumbukumbu za ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey
Zambi wakikagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya pango la ardhi mkoani Lindi
Ndugu Gibson Mwaigomole Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) Lindi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Lukuvi ameamuru kusimamishwa kazi Afisa Mipango Miji wa Lindi Ndugu
Castory Manase Nkuli baada ya kunyang`anya ardhi ya vijiji vya Ruvu na Mchinga
hekari 4000 na kumilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate kinyume cha sheria
ya Ardhi.
Mhe. Lukuvi aligundua hayo baada ya kuona utaratibu
wa umilikishaji wa ardhi haukufuatwa na badala yake kuonekana kuwa
na mianya ya rushwa kwa kuwa ardhi hiyo imehamishwa kutoka ardhi ya kijiji hadi
kumilikishwa kwa kampuni ya Azimio ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo
itoke kwa idhini ya Rais.
Aidha, Afisa Mipango Miji huyo aligundulika kuwa na
kosa la kughushi kwa kujifanya ni Afisa ardhi baada ya kuandika barua na
kuisaini kwa niaba ya Afisa ardhi wakati yeye ni Afisa Mipango Miji ili
kuimilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate ambalo pia ni kosa kisheria.
Akithibitisha makosa hayo Kaimu Mkurugenzi Mipango
Miji na Vijiji kutoka Wizara ya Ardhi Bi Immaculate Senje amesema kwamba
utaratibu wa umilikishaji wa ardhi hiyo haukufuatwa ambapo kisheria ilitakiwa
hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais na baada ya Tangazo la Serikali na
kuridhiwa na wana kijiji.
“Kama nyie hamna uwezo wa kumfukuza kazi basi
mie namsimamisha kazi kuanzia leo hafai kuwa mtumishi wa serkali” alisema Mhe.
Lukuvi na kuagiza eneo hilo lirudi na kuwa mali ya serikali “ Sasa hiyo ardhi
lazima irudi itakua mali ya serikali kuanzia leo” .
katika ziara hiyo, Mhe. Lukuvi ametembelea ofisi za
ardhi Lindi na kufanya ukaguzi katika Masijala za ardhi na kuangalia mfumo wa
ukusanyaji kodi ya pango la ardhi, kisha kuwaagiza watendaji wa ardhi mkoani
hapo kuhakikisha wanatoa hati kwa wakati na kukusanya kodi ya pango la ardhi
kwa kila mmiliki wa ardhi ili kuongeza pato la serikali.
Pia alitembelea ofisi za Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) mkoani hapo na kupokea taarifa kutoka kwa Meneja wa shirika hilo mkoani
Lindi Ndugu Gibson Mwaigomole. Katika taarifa hiyo Mhe. Lukuvi amelishauri
Shirika la Nyumba la Taifa kufanya uwekezaji mkoani Lindi kwa kujenga ofisi za
kisasa pamoja na Nyumba zenye gharama nafuu.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi
akiwa pamoja na waziri Lukuvi na watendaji wa mkoa ameeleza kuwa sekta ya ardhi
mkoani hapo inachangamoto nyingi lakini ofisi yake inaendelea kufanya jitihada
za makusudi kuhakikisha changamoto hizo zinapungua au kuzimaliza kabisa kwa
maslahi ya watu wa Lindi na Tanzania kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment