Afisa habari wa Azam
Jafar Iddy (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa
kumtambulisha mshambuliaji yao mpya Waziri Junior (wa pili kushoto) aliyesaini
kandarasi ya kuitumikia klabu hiyo.
Aliyekuwa mshambuliaji wa timu ya Toto Afrika Waziri Junior
ametambulishwa leo mbele ya waandishi wa habari baana ya kusaini kandarasi na
timu ya Azam.
Azam jana walifanikiwa kupata saini ya mshambuliaji huyo kinda kutoka
Toto ikiwa ni katika muendelezo wa kuboresha kikosi chao ili kuweza kufanya
vizuri katika msimu ujao unaokuja.
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa habari wa Azam Jafar Iddy
amesema kuwa wamefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji juyo kinda kutoka Toto
kwani hilo limekuja ikiwa ni moja ya mapendekezo ya kocha mkuu wa timu hiyo.
"huu ni muendelezo wa kusajili na kufa nya marekebisho katika
kikosi chetu kuelekea msimu ujhao, na usajili huu unakuja baada ya kuona
mapendekezo ya kocha mkuu Aristoc Cioaba na akwa sasa ni kuwapa fursa
vijana,"amesema Iddy
Awali Waziri alikuwa anawaniwa na timu Yanga lakini Azam wameonekana
kuwapiga bao na kumsainisha kwa dau nono.
No comments:
Post a Comment