Kufuatia kifo cha mmoja wa Waasisi wa CHADEMA, Mzee
Philemon Ndesamburo Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,
(CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji, ametoa maelekezo kwa watendaji nchi nzima
kupeperusha bendera nusu mlingoti
Mashinji ametoa maelekezo hayo leo wakati akiongea
na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam na
kusema bendera zinapaswa kupeperushwa nusu mlingoti hadi mwili wa kiongozi huyo
utakapopumzishwa katika nyumba yake ya milele.
"Chama kitashiriki katika msiba huu kwa heshima
zote kumuenzi mmoja wa waasisi wa siasa za mabadiliko ya kweli na Uhuru wa
kweli nchini, msiba huu ni msiba wa CHADEMA, ni msiba wa Watanzania, ni msiba
wa Taifa letu kutokana na mchango mkubwa wa Mzee wetu kisiasa, kiuchumi na
kijamii kwa nchi yetu, Mhe. Ndesamburo ndiye aliyekifadhili Chama kwa mara ya
kwanza kwa kukipatia ofisi eneo la Kisutu jijini Dar es salaam" amesema
Dkt. Mashinji
Nyumbani kwa
Marehemu Mzee Philemoni Ndesamburo aliyefariki dunia katika Hosptali ya
Rufaa ya KCMC mjini Moshi.
Baadhi ya
waombolezaji wakiwemo ndugu wakijiandaa kwenda kutizama mwili wa Mzee
Ndesamburo katika HospItali ya Rufaa ya KCMC.
Baadhi ya
Waombolezaji wakiwemo Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakia
nyumbani kwa Mzee Ndesamburo.
Mbunge wa jimbo la
Arusha Mjini, Godbless Lema pamoja na mkewe Neema Lema wakiwasili nyumbani kwa
marehemu Mzee Ndesamburo.
Mbunge wa jimbo la
Arusha mjini, Godbless Lema akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Rombo, Joseph
Selasini mara baada ya kukutana nyumbani kwa marehemu Mzee Ndesamburo .
Mtoto wa Marehemu
Ndesamburo, Ndohorio Ndesamburo akiwaeleza jambo waombolezaji waliofika
nyumbani kutoa pole kwa familia.
Mwenyekiti wa
Chadema kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa akitia saini katika kitabu cha
waombolezaji nyumbani kwa marehemu Ndesamburo.
Baadhi ya viongozi
wa Chadema wakiwa katika kikao kifupi nyumbani kwa mareheu Ndesamburo.
Familia ya marehemu
Ndesamburo wakiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya KCMC
kwa ajili ya kutizama mwili wa mpendwa wao.
Mkurugenzi wa
kampuni ya World Frontier, John Hudson akimfariji, mtoto wa marehemu
Ndesamburo, Lucy Owenya nyumbani kwao eneo la Mbokomu mjini Moshi.
Baadhi ya
waombolezaji wakiwafariji wafiwa.
No comments:
Post a Comment