Mwanamke mmoja alikwenda kwa Mchungaji wa MUNGU
kumlalamikia kuwa mumewe anawaalika wageni wengi nyumbani kwao kiasi cha kwamba
amechoka kuwapikia na kuwahudumia.
Mchungaji hakumjibu kitu na yule mwanamke
akaondoka.
Siku
moja Mchungaji alimwita mume wake yule mwanamke na kumwambia "Mimi leo
nitakuwa mgeni wako".
Yule
Bwana alifurahi sana na akaenda kwa mkewe na kumwambia "Mchungaji mtumishi
wa Mungu atakuwa mgeni wetu leo".
Yule
mkewe kusikia hivyo akafurahi na kumfanyia matayarisho na mapishi mazuri kwa
mgeni wao mchungaji.
Baada
ya makaribisho mema aliyoyapata Mchungaji akamwambia yule Bwana "Mwambie
mkeo autazame mlango mimi nitakao ondokea".
Hivyo
yule mwanamke akautazama mlango ambao Mchungaji mtumishi wa Mungu aliondokea
akaona viumbe wote wabaya wakiondoka nyumbani kwao na kumfuata Mchungaji nyuma
yake.
Yule
mwanamke kuona hivyo kiasi ambacho alizimia kutokana na maajabu aliyo yaona.
Baadae
yule mwanamke alikwenda tena kwa Mchungaji , akamwambia uliona nini baada ya
mimi kuondoka mlangoni pale nyumbani kwenu..
Mwanamke
akamwambia yote aliyoyaona alivyoondoka....
Mchungaji
akamwambia "Hivyo ndivyo inavyotokea, mgeni huondoka na mabaya yote ya
nyumba na viumbe vyote vibaya.
Hii
ndio hekima ya Mwenye nyumba kumhudumia na kumpikia mgeni wake mpaka mwenye
nyumba akachoka."
Nyumba
ambayo hupata wageni wengi ni nyumba ambayo Mungu Baba anaipenda.
Hakuna
kizuri kama nyumba iliyo wazi kwa watoto na wazee. Nyumba ya namna hii hupata
huruma na baraka kutoka kwa Mungu Baba.
Bwana
amesema kama Mungu Baba Akitaka kuwapatia wema watu wake, huwapelekea zawadi.
Wanafunzi
wake Wakamuuliza " Ni zawadi gani hiyo ewe Mwalimu ?" Akawajibu
"mgeni huja na vyakula vyake na huondoka na dhambi za wenyeji wake."
Hivyo
ndugu zangu..kuwa mkirimu kwa wageni ni njia mojawapo ya kumpendeza Mungu Baba.
No comments:
Post a Comment