Manchester
United ndio klabu yenye thamani kubwa barani Ulaya ikiwa na thamani ya Yuro
bilioni 3 kulingana na kampuni ya biashara ya KPMG.
Mabingwa hao wa kombe la
Yuropa wanaongoza katika orodha ya thamani ya Kampuni ya KPMG, ikiwa mbele ya
mabingwa wa Uhispania Real Madrid na Barcelona.
Utafiti huo uliangazia
haki za kupeperusha matangazo, faida, umaarufu, uwezo kimchezo na umiliki wa
uwanja.
Katika utafiti huo uliofanyiwa timu 32, vilabu vya Uingereza vilitawala orodha hiyo vikijaza nafasi sita kati ya 10 bora.
Katika utafiti huo uliofanyiwa timu 32, vilabu vya Uingereza vilitawala orodha hiyo vikijaza nafasi sita kati ya 10 bora.
Andrea Sartori ambaye ni
mkurugenzi wa maswala ya michezo katika kampuni ya KPMG amesema kuwa kwa jumla
thamani ya soka imekuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
''Huku hilo likielezewa
kufuatia kuimarika kwa matangazo, operesheni za biashara za kimataifa,
uwekezaji wa vifaa vya umiliki wa kibinafsi, vifaa vya kisasa pamoja na
usimamizi mzuri ni vigezo muhimu vya ukuaji huo'', alisema.
Kuhusu haki za matangazo,
ligi kuu ya Uingereza inaongoza ligi nyengine za Ulaya ijapokuwa ligi nyengine
zimeweka mikakati kupigania mashabiki wa kimataifa.
Vilabu kumi bora vyenye
thamani ya juu kibiashara:
1. Manchester United -Euro3.09bn
2. Real Madrid - Euro2.97bn
3. Barcelona - Euro2.76bn
4. Bayern Munich - Euro2.44bn
5. Manchester City - Euro1.97bn
6. Arsenal - Euro1.95bn
7. Chelsea - Euro1.59bn
8. Liverpool - Euro1.33bn
9. Juventus - Euro1.21bn
10. Tottenham - Euro1.01bn
No comments:
Post a Comment