MABINGWA Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom (VPL) Yanga leo wameaga
amashindano ya SportPesa Super Cup kwa mikwaju ya penati 4-2 katika mchezo wa
hatua ya nusu fainali yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es
Salaam.
Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Uhuru ulianza majira ya saa 8
kamili kwa kuzikutanisha timu ya Yanga dhidi ya AFC Leopard ya nchini Kenya.Mpaka
dakika 90 za mpira zinamalizika timu hizo zilitoshana nguvu kwa kutoka suluhu
na kuelekea kwenye mikwaju ya penati.
Timu zote zilionekana kushambulia kwa kupokezana lakini safu za
ushambiaji hazikuwa makini na kupoteza nafasi walizozipata mara kadhaa.
Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Emanuel Martin na kuingia Said
Musa, akatoka Maka Edward na kuingia Said Makapu, Yusuph Mhilu alitoka na
kuingia Samwel Greyson na Pato Ngonyani alitoka na kuingia Babu Ally.
AFC Leopard wakafanya mabadiliko kwa kumtoa Abwao Marcus na kuingia
Ingotsi Marselas.
Wachezaji waliopiga penati kwa upande wa Yanga ni Nadir Haroub, Obrey
Chirwa ambao walipata na Said Makapu na Said Musa kukosa kwa upande wa
Yanga.Kwa upande wa AFC Leopard ni golikipa Jan Otieno, Otieno Duncan, Bernad
Mango na Katerega Allan ambao walipata na Ingotsi Marselas alikosa.
Beki
wa Yanga, Juma Abdul, (kulia) akiruka kuwania mpira na beki wa AFC Leopards
Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super
Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo. Katika mchezo
huo AFC Leopards wameibuka na uwashinda wa mikwaju ya penati 4-2 baada ya
kumalizika dakika 90 kwa sare ya 0-0.
Mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi (kulia)
akiwania mpira na Kiungo wa AFC Leopards, Alan Katerega, wakati wa mchezo Nusu
Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru
jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji
wa Yanga Juma Mahadhi (kulia) akimtoka mpira na beki wa AFC Leopards, Abdallah
Salim, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup,
uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji
wa Yanga Obrey Chirwa, akijiandaa kupiga shuti huku akizongwa na mabeki wa AFC
Leopards, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup,
uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji
wa Yanga Juma Mahadhi (kulia) akimtoka mpira na beki wa AFC Leopards, Abdallah
Salim, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup,
uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji
wa Yanga, Juma Mahadhi (kushoto) akichuana kuwania mpira na Abdallah Salim,
wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa
kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Mhilu
akimkalisha beki wa AFC Leopards
No comments:
Post a Comment