Ilikuwa ni tetesi lakini sasa ni
‘DoneDeal’ baada ya klabu ya Simba kumsaini golikipa huyo kutoka klabu ya Azam
FC.
Manula amesaini mkataba wa miaka
miwili kuitumikia Simba kwa dau la shilingi milioni 50 za Tanzania.
Awali kulikuwa na minong’ono kwamba
Manula ambaye ni mshindi wa tuzo ya golikipa bora VPL msimu uliopta amesaini
kujiunga na Simba lakini klabu ya Azam kupitia kwa afisa habari wao Jafar Idd
walikanusha taarifa hiyo na kusisitiza Azam ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na
Manula ili kumuongeza mkataba.
Manula anakua mchezaji wa pili
kujiunga na Simba akitokea Azam baada ya awali John Bocco kuondoka kwenye klabu
hiyo na kuelekea Msimbazi akiwa mchezaji huru.
No comments:
Post a Comment