Vyombo vya habari nchini humo,
vinasema kuwa vyakula na mimea mashambani imevamiwa na kulazimu mamlaka kuu
nchini humo kuamua kuwalipa wananchi senti 4 kwa kila panya atakayeletwa kwa
mamlaka akiwa ameuwawa.
Wanakijiji katika eneo la Ayeyarwady
wamekuwa wakikabiliana na uvamizi huo wa panya kwa kuwaulia mbali wanyama hao
ambao wamewavamia kwa wingi katika kipindi cha siku kumi zilizopita.
Maafisa wakuu wa eneo hilo wamelaumu
mvua kubwa inayonyesha kwa sasa, jambo lililosababisha ongezeko kubwa la panya,
huku wakivamia hifadhi ya chakula katika maghala ya wanakijiji.
Panya wengi wamepatikana kwenye nyumba
20, zilizoko karibu na vijiji vya Zee Chai village pwani ya manispaa ya Nga Pu
Taw.
Kufikia sasa panya 800 wameuawa, huku
waliosalia wamekimbilia msitu ulioko karibu.
Hayo ni kwa mjibu wa wakazi wa eneo
hilo.
Wananchi wanahofia kupatwa na maradhi
yanayosababishwa na panya.
Ili kubaini ikiwa panya hao wana
virusi vya ugonjwa mmbaya na bakteria, panya wanaokamatwa wakiwa hai au
waliokuwa hupelekwa kwenye maabara ya idara ya afya iliyoko mjini Yangon, hayo
ni kulingana na idara ya afya katika jimbo hilo la Ayeyarwady.
Kwa mjibu wa Wizara ya Habari, panya
wengi pia wameonekana wakiingia katika vijiji vya kisiwa cha Haigyi, mahali
ambapo zaidi ya panya 1,600 wameuliwa.
Mnamo mwaka 2004, panya walivamia na
kula kila kitu katika kijiji cha Pathein, makao makuu ya jimbo la Ayeyarwady,
kutokana na ukosefu wa chakula, lakini hakuna aliyeambukizwa maradhi yatokanayo
na panya.
No comments:
Post a Comment