Msimu ulioisha
wa ligi pamoja na kuwekeza pesa nyingi sana katika usajili na kununua baadhi ya
wachezaji wakubwa lakini klabu ya Ufaransa ya PSG ilishuhudia ikipoteza kombe
la Ligue 1 ambapo kombe hilo lilienda kwa timu ya Monaco.
Patrick Kluivert
alikuwa mkurugenzi wa masuala ya ufundi katika timu hiyo na ameamua kubwaga
manyanga, Kluivert ambaye ameshawahi kuvichezea vilabu vya Ajax,Ac Millan na
Barcelona amedumu katika ukurugenzi huo kwa muda mfupi wa msimu mmoja tu.
Haijawekwa wazi
sana sababu za Kluivert kubwaga manyanga lakini inaonekana wazi wazi kwamba
kitendo cha Monaco kuumaliza ubabe wa PSG na matokeo yao katika Champions
League ndio sababu kubwa kwa Kluivert kuachia ngazi kwani hata mabosi wa timu
hiyo hawakufurahishwa na mwenendo wa timu hiyo tangu Kluivert apewe jukumu
hilo.
Raisi wa klabu
ya PSG Nasser Al Khelaifi amesema kocha wa klabu hiyo Emery atabaki kuwa kocha
wao lakini akimshukuru Kluivert kwa kazi aliyoifanya akiwa klabuni
hapo”tunamshukuru Patrick kwa kazi kubwa aliyofanya akiwa na sisi na tunamtakia
kila la kheri kwa kile alichoamua kukifanya katika miaka ijayo” alisema
Khelaifi.
Msimu huu PSG
wameshinda Coupe de France na Coupe de la Ligue pekee matokeo ambayo hayakuwa
mazuri na yalimfanya Kluivert na kocha Unai Emery kuonekana kama wanaiangusha
timu na hivyo Patrick Kluivert kuamua kuachana na timu hiyo.
No comments:
Post a Comment