Salum Mayanga kocha mkuu wa kikosi cha
Stars hakubaliani kabisa na wanaosema au kudhani kwamba, timu ya taifa ya
Lesotho ni ‘kibonde,’ Mayanga anaami kuwa kwenye mashindano hakuna timu
kibonde.
Mayanga anachoamini yeye ni kwamba
Stars ilishindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Lesotho baada ya kuruhusu goli
rahisi la kusawazisha na badae kubanwa na kushindwa kutengeneza nafasi za
kutosha kuongeza magoli mengine.
“Kwanza lazima tukubali kwenye
mashindano hakuna timu ‘kibonde’ lakini tulitangulia kufunga goli, leo
tumecheza mchezo wa kushambulia tukiwa na washambuliaji watatu ndio ulikuwa
mpango wetu lakini tumefanya makosa tumeruhusu goli rahisi la kusawazisha.”
“Matokeo ya sare kwa nyumbani si
mazuri lakini ndio matokeo ya mchezo yaliyotokea kwa siku ya leo, tulianza game
vizuri kwa kutangulia kufunga goli kwa bahati mbaya hatukuwa makini tukawapa
nafasi kirahisi wakaweza kusawazisha goli baada ya hapo walitengeneza ulinzi wa
kutosha ikatupa wakati mgumu wa kuweza kutengeneza nafasi kufunga goli la
pilina kuongoza la tatu.”
“Kwa upande wangu ni changamoto kosa
lililojitokeza la kuruhusu goli lirudi nadhani tutapata muda wa kufanya
marekebisho na kuona mechi zinazofuata tunafanya vizuri zaidi.”
“Baada ya wao kupata goli la
kusawazisha, wakafunga eneo lao la nyuma ikawa kasi sisi kupata nafasi ya
kufunga goli lingine.”
Maynaga pia amesema, kushindwa kupata
matokeo ya ushindi kwenye mechi dhidi ya Lesotho si kwamba ndio mwisho wa
safari ya Stars kufuzu kwenda kucheza fainali za AFCON.
“Bado tutaendelea kufanya mazoezi na
kurekebisha makosa tuliyofanya ili michezo inayokuja tuone nini kitatokea.”
No comments:
Post a Comment