Wakati Azam ikiendelea kunyakua
wachezaji kutoka Kanda ya Ziwa, Simba imeendelea kuibomoa Azam na hiyo ni baada
ya kufanikiwa kumrejesha mlizi wao wa zamani Shomari Kapombe.
Kapombe amesaini mkataba wa miaka
miwili kuitumikia Simba lakini bado haijajulikana ni kwa kiasi gani cha fedha.
Mlinzi huyo wa Taifa Stars anarejea
kwa mara nyingine kwenye klabu yake ya zamani ambayo ilimtoa na badae akaenda
kucheza soka la kulipwa Ufaransa lakini hakudu na aliporejea akajiunga Azam FC.
Kapombe anafanya idadi ya wachezaji wa
Azam waliojiunga na Simba kufikia watatu akiungana na John Bocco ‘Adebayor’ na
Aishi Manula.
No comments:
Post a Comment