Kwa mara ya kwanza kuanzia mwaka 1966
Waingereza wameshinda kombe kubwa la dunia baada ya timu yao ya vijana chini ya
miaka 20 kuibuka kidedea katika mchezo wa fainali dhidi ya Venezuela.
Hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa
Waingereza kucheza fainali kubwa ya dunia toka miaka 51 iliyopita walipocheza
na kushinda kombe la dunia na hii ni faraja kwao kama Waingereza kutokana na
matokeo yasiyoridhisha ya timu yao ya wakubwa.
Alikuwa Dominic Calvert katika kipindi
cha kwanza ambaye aliiandikia Uingereza bao la kuongoza na la pekee katika
mchezo lakini pia shukrani zimuendee mlinda mlango wa Uingereza Freddie
Woodmans ambaye aliokoa mkwaju wa penati kipindi cha pili.
Golikipa wa Uingereza alikuwa nyota wa
mchezo huo kwani Venezuela walimuandama sana kwa mashambuli na shuti la
mshambuliaji wao Lucena liligonga mwamba shambulizi ambalo lilikuwa hatari
zaidi kwa Waingereza lakini walijitahidi na kuibuka kuidedea katika fainali
hiyo.
No comments:
Post a Comment