Meneja wa Mwalimu Commercial Bank, Plc, (MCB), tawi la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, Bi. Leticia Ndongole, (wapili kushoto), akimkabidhi zawadi ya IPAD, Bw. Khamisi Mmuka, kutoka wilayani Newala mkoani Mtwara, baada ya kuibuka mshindi kwenye droo ya kampeni ya "weka akiba na ushinde" iliyochezeshwa na benki hiyo. Anayeshuhudia ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa.
Meneja Masoko wa MCB, Bi. Rahma Ngassa, akizungumza na waandishi wa habari baada ya zoezi la kutoa zawadi.
Mshindi wa vocha ya manunuzi, Bi. Macrina Yoram Kyando, (kushoto), kutoka wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, akielezea furaha yake baada ya kuibuka mshindi.
Mshindi wa vocha ya manunuzi, Bi. Flora Mbaule, (kushoto), kutoka wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, akielezea furaha yake baada ya kuibuka mshindi.
Afisa wa Huduma kwa wateja wa MCB, Bi.Martha Gambosi, (kushoto), akimkabidhi vocha ya manunuzi mshindi wa kampeni ya "weka akiba na ushinde" Bi. Flora Mbaule kutoka wilayani Temeke.
Meneja wa tawi la Samora wa MCB, Bi. Leticia Ndongole, (Kushoto), akimpongeza Bi. Flora Mbaule kwa ushindi wake uliompatia zawadi.
Kiongozi wa watumishi wa MCB tawi la Samora, Bw.Ombeni Kaale, (wapili kulia), akimkabidhi zawadi ya vocha ya manunuzi, Bi. Macrina Yoram Kyando, kitoka wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, baada ya kuwa miongoni mwa washindi wa droo ya "weka akiba na ushinde" iliyochezesha na MCB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa, (wakwanza kushoto) na Menja wa tawi la MCB, Samora, Bi. Leticia Ndongole.
Na Khalfan Said
BENKI ya Mawlimu, (Mwalimu Commercial Bank plc),
imewakabidhi zawadi washindi watatu wa kampeni ya “weka akiba na ushinde’
ambapo mteja wa benki hiyo kutoka wilayani Newala, Bw.Khamisi Mmuka,
alijinyakulia zawadi ya IPAD.
Katika hafla hiyo ya kukabidhi zawadi iliyofanyika
alasiri ya Agosti 7, 2017 kwenye tawi la Samora la benki hiyo, washindi wengine
ni Bi.Flora Mbaule na Bi.Macrina Yoram Kyando wote kutoka Temeke jijini Dar es
Salaam ambao walijnyakulia vocha za manunuzi.
Akizungumza kweney hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Meneja Masoko wa MCB, Bi. Rahma Ngassa alisema, kampeni hiyo ilianza Mei 18, 2017 ambapo mteja mwenye akaunti kila anapoweka akiba ya fedha kiasi cha shilingi elfu hamsini (50,000) kwenyeakaunti yake, aliingia moja kwa moja kwenye droo hiyo. “Na sio mteja wetu tu hata mwananchi aliyefungua akaunti na kuweka kiasi kama hicho cha fedha naye pia alipata fursa ya kushiriki.” Alifafanua Bi. Rahma.
Akizungumza kweney hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Meneja Masoko wa MCB, Bi. Rahma Ngassa alisema, kampeni hiyo ilianza Mei 18, 2017 ambapo mteja mwenye akaunti kila anapoweka akiba ya fedha kiasi cha shilingi elfu hamsini (50,000) kwenyeakaunti yake, aliingia moja kwa moja kwenye droo hiyo. “Na sio mteja wetu tu hata mwananchi aliyefungua akaunti na kuweka kiasi kama hicho cha fedha naye pia alipata fursa ya kushiriki.” Alifafanua Bi. Rahma.
Naye Meneja wa tawi la Samora wa benki hiyo,
Bi.Leticia Mmuka, alisema ingawa kampeni hiyo imemalizika lakini amewahimiza
wananchi kufungua akaunti kwenye benki hiyo na wale wenye akaunti waendelee
kuweka fedha zao kwani benki inatoa huduma bora na zenye kuvutia wateja.
Alisema huduma huizo ni pamoja na kutoa gharama
nafuu na rafiki za kibenki na ni sukuhisho la kifedha kwa walimu, watumishi wa
serikali, wafanyabiashara, wakulima na wananchi kwa ujumla.
“Huduma za kibenki zitolewazo na MCB ni pamoja na
mikopo yenye riba nafuu, huduma ya ATM iliyounganishwa na mtandao mpana wa
UMOJA SWITCH uliosambaa nchi nzima.” Alifafanua zaidi.
Aidha kwa upande wao washindi wa zawadi hizo
walisema, wamefurahishwa na jinsi benki inavyowashirikisha wananchi na wateja
kwenye kampuni kama hiyo na kuwataka wananhi kufungua akaunti na benki hiyo
ambapo huenda nao wakapata zawadi kubwa zaidi ya walizopata wao.
“Nimefurahi sana kushinda zawadi hii, kwani mimi ni
mteja wa MCB kutoka mbali kidogo, hko Neawala mkoani Mtwara, laini nimeibuka
mshindi, nah ii inaonyesha hapakuwepo na upendeleo wowote, nawashukuru sana MCB
kwa zawadi hii.” Alisema mshindi wa IPD Bw. Khamisi Mmuka.
No comments:
Post a Comment