Mganga mkuu wa mkoa wa dar es salaam Dr. Grace Maghembe(kushoto)akizungumza na waandishi wa habari.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amewataka wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upimaji Afya litakalo anza siku ya jumatano asubuhi ya juma hili.
Amesema magonjwa mbalimbali yakuambukizwa na yasiyo ya kuambukizwa yatapimwa na wataalamu wa afya kutoka Hospitali kubwa hapa nchini, ambapo wataalamu Zaidi ya 200 watahudumia wananchi katika zoezi hilo.
Serikali ya mkoa tumejipanga kuhudumia secta ya Afya lakini hatuwezi kujua mahitaji halisi ya madawa bila wananchi kupima afya zao, tukijua tutajipanga vizuri kupunguza pia vifo vya mama na mtoto, pia nawaomba tuwe na utamaduni wa kupima afya.
“Wale wote watakaohudumiwa wakigundulika na matatizo makubwa watapata rufaa ya kwenda katika hospital kubwa kwaajili ya kuendelea na matibabu“ Alisema Makonda
Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Grace Maghembe amesema Zoezi hili Lita anza jumatano hadi Jumapili, katika viwanja vya mnazi mmoja, amesema wameamua kushirikiana wadau wa Hospital za serikali na Binafsi ambazo ni Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya .Amana,Temeke,Mwananyamala, TMJ, Agakhan ,Regency, Damu salama ,Shirika la MDH na wengine wengineo.
Makonda amesema kuwa hatopenda kuona Mwananchi anapoteza maisha kwa kukosa huduma ya Afya ndio maana ameamua kuendesha zoezi la upimaji wa Afya Bure ili Wananchi wapate fursa ya kujua Afya zao na kuwa na utaratibu wa kupima Afya zao mara kwa mara.
Aidha amezipongeza Hospitali zilizomuunga mkono ikiwemo Muhimbili, Ocean Road, Amana, Temeke, Mwananyamala, Muhimbili, TMJ, Sanitas, Agha Khan, Regency, Kairuki, TANCDA, IMMI Life, APHTA, CCP Medicine, MDA, NHIF, Wandile wa kaya, P Consult, Besta Diagnestics, Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, Jamii Bora na Damu salama.
No comments:
Post a Comment