DC KINONDONI AZINDUA ZOEZI LA UPIMAJI WA VIWANJA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, March 25, 2018

DC KINONDONI AZINDUA ZOEZI LA UPIMAJI WA VIWANJA

IMG_0044
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi, akihutubia wananchi wa kata ya Nyakasengwe alipokwenda kuweka jiwe kwaajili ya uzinduzi rasmi wa upimaji wa viwanja katika kata hiyo.
IMG_0057
IMG_0060

IMG_0065
IMG_0102
 Baadhi ya wananchi walioudhulia katika hafla hiyo.
IMG_0107
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi, wa (pili kushoto) akiweka jiwe kuashiria uzinduzi huo wengine ni Viongozi wa serikali za mtaa huo.

Takribani viwanja 5000 vilivyoko Kata ya wazo eneo la Nyakasangwe Wilaya ya Kinondoni, vimepimwa nje ya bajeti ya Serikali, baada ya kutatuliwa kwa uliokuwa mgogoro wa muda mrefu uliohusisha wakaazi wa eneo lile pamoja na wenye mashamba.


Akiongea na wananchi wa eneo hilo,baada ya uzinduzi wa upimaji, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi amesema amefurahishwa sana kwa mgogoro huu uliogharimu maisha ya watu kumalizika kwa kiwango na manufaa makubwa yenye tija kwa Taifa letu.


Amesema migogoro kama hii imekuwa changamoto kubwa ya amani katika Nchi yetu, hasa Wilaya ya Kinondoni inayohitaji hekima, busara, majadiliano ya kina, na masikilizano katika utatuzi wake.


Akitoa taarifa ya upimaji wa viwanja hivyo Mkurugenzi kutoka kampuni ya Afro Map Ltd iliyoendesha zoezi hilo la upimaji Ndg Fransis Mkwela amesema wamefanikiwa kupima maeneo ya wazi, maeneo ya shule ya Sekondari, maeneo ya viwanda vidogo vidogo, na maeneo ya nyumba za kuabuduia.


Maeneo mengine ni kituo cha polisi, maeneo ya Umma, eneo la kituo cha Afya, eneo la zahanati na eneo la shule ya Msingi.


Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyakasangwe Ndg Peter Belebela akimkaribisha Mkuu huyo wa Wilaya kwenye uzinduzi huo ameushukuru uongozi mzima kwa jitihada zilizofanyika kumaliza mgogoro huo na kuwataka wanachi wake kuheshimu zoezi hilo lá upimaji unaoendelea pamoja na miundo mbinu ya barabara na mipaka.

Mkutano huo umefanyika katika eneo la shule ya Msingi Nyakasangwe uliohusisha wananchi wa eneo hilo pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages