Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya ugonjwa wa kifua kikuu.
Kikundi cha ngoma wakiendelea kucheza na kuimba nyimbo mbalimbali zenye kuelimisha kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu katika Manispaa ya Ilala.
Katibu wa kikundi cha Tokomeza Kifua Kikuu na Ukimwi (TOKIKUTA) wa kwanza kutoka kushoto Bi. Tapu Junia kifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema kuhusu majukumu ya kikundi hicho katika kuhakikisha wanaelimisha jamii na kutomeza ugonjwa wa kifua kikuu. ambapo alieleza kuwa kikundi hicho kipo kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma pamoja na kuhamasisha kwenda kupima magonjwa mbalimbali.
Kikundi cha TOKIKUTA wakicheza ngoma.
Wapiga ngoma wakitekeleza majukumu yao katika maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa kifua kifua kikuu Manispaa ya Ilala.
Waigizaji wakiingiza muhimu wa kwenda hospitali kupima magonjwa mbalimbali badala ya kwenda kwa mganga wa kienyeji.
Baadhi ya wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wakimsindikiza mgeni rasmi katika maandhimisho hayo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Mjema
Baadhi ya viongozi waliohudhulia katika hafla hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akisalimiana na Makamu Mwenyekiti tokomeza kifua kikuu (TOKIKUTA) Pulina Mgata, katika hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema (wapilikushoto) akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa tokomeza kifua Kikuu (TOKIKUTA) Tabu Juma
Watanzania wametakiwa kuwa na ushirikiano katika kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa wa kifua kikuu ambao umeonekana sio rafiki kutokana na kugharimu maisha ya watu.
Akizungumza katika maadhimisho ya Ugonjwa wa Kifua kikuu katika Manispaa ya Ilala, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema amesema kuwa ugonjwa huo unapaswa kupigwa vita na kila mtu.
Mhe. Mjema ambaye ni mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, amesema kuwa ni vema kila mtu anamlinde mwezake jambo ambalo litasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wa kifua kikuu hapa nchini.
" Wilaya ya Ilala sasa inatakiwa kuanzisha kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu kwenda kwa mtu mwengine" amesema Mhe.Mjema.
Ameeleza kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitema mate hovyo, bila kujua kufanya hivyo kunaweza kuchochea ongezeko la ugonjwa wa kifua kikuu kutokana ugonjwa huo unaambukiza kwa njia ya hewa.
"Imefika wakati kupiga vita vitendo hatarishi kwa afya ikiwemo kuuza vyakula pamoja matunda ambayo hayajaifadhiwa sehemu salama ili kuepuka magonjwa" amesema Mhe. Mjema.
Mganga Mkuu wa Ilala amebainisha kuwa kwa mujibu wa shirika la afya duniani, Tanzania inashika nafasi ya sita kuwa watu wenye ugonjwa wa kifua kikuu, huku Afrika ikiwa nafasi ya nne.
Ameseme kuwa katika Wilaya ya Ilala kuna maeneo ambayo yanaongoza kuwa na wagonjwa wengi wa kifua kikuu ambayo ni Kata ya Buguruni, Ukonga, Kiwalani pamoja na Vingunguti.
Imeelezwa kuwa kata hizo zinachangia asilimia 80 kwa wagonjwa wenye kifua kikuu ambao wanagundulika takribani 5,000 kila mwaka.
Manispaa ya Ilala wameadhimisha leo siku ya wagonjwa wa kifua kikuu katika kata ya Mchikichini jijini Dar es Salaam wakiwa na kauli mbiu ya mwaka huu ‘Viongozi tuwe mstali wa mbele kuongoza mapambano ya kutokomeza kifua kikuu’.
No comments:
Post a Comment