Afisa Mtendaji Mkuu wa TMJ Hospital, Bi. Parul Chhaya, akiongea wakati wa halfa ya kuwafariji wagonjwa wa figo, iliyoandaliwa na Hospital ya TMJ—kama sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wagonjwa wa Figo, Syed Chambala, katika ni Mkurugenzi Mkuu wa TMJ Hospital, Dk. Tayabal Jafferji,Mkurugenzi Mkuu wa TMJ Hospital, Dk. Tayabal Jafferji, akiongea wakati wa halfa ya kuwafariji wagonjwa wa figo, iliyoandaliwa na Hospital ya TMJ—kama sehemu ya Maadhimisho wa Siku Figo Duniani. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wagonjwa wa Figo, Syed Chambala.
Daktari Msaafu Martini, Sebalua ambae ni mgonjwa wa figo akiongea wakati wa halfa ya kuwafariji wagonjwa wa figo, iliyoandaliwa na Hospital ya TMJ—kama sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani.
Wagonjwa wa figo nchini wameiomba serikali ya awamu ya tano kuongeza juhudi kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa figo kwa kupeleka huduma na vifaa katika hospitali za mikoani na wilayani.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya figo duniani iliyoandaliwa na hospitali ya TMJ, Mwenyekiti wa wagonjwa wa figo wanaotibiwa katika hospitali hiyo, Ndugu Syed Chambala alisema ni muhimu kwa serikali kuweka mkazo wa kupambana na ugonjwa huo.
“Ugonjwa wa figo bado haujawekea mkazo wa kutosha na serikali yetu kwa sababu huduma na vifaa vya kusafishia figo bado vinapatikana mjini Dar es Salaam pekee na inawalazimu wagonjwa kutoka mikoani kuingia gharama kubwa ili kuweza kupata matibabu hayo,” aliongeza
Ndugu Chambala alisisitiza kwamba lazima kuwe na kipaumbele katika kupambana na ugonjwa wa figo nchini na ni muhimu kukawa na utaratibu wa kupatikana na fedha ili wagonjwa wa mikoani waweze kusafirishwa.
Alisistiza kwamba ni muhimu serikali ikapanua wigo wa huduma na matibabu ya figo ili kupunguza mzigo kwa wagonjwa wanaopaswa kusafiri kuja jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
“Kwa kweli huduma za hospitali hii ya TMJ ni za kuridhisha sana kwa wagonjwa wa figo na kitengo chao cha huduma hii kipo imara ( Dialysis Unit) na upatikanaji wa dawa hospitali hapo ni wa asilimia 90,” alieleza kwa wanahabari waliohudhuria shughuli hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Dkt Tayabali Jafferji alisema kwamba hospitali hiyo imeungana na jumuiya za kimataifa katika kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo ambao unakua kwa kasi duniani.
Aliongeza kwamba hospitali yao inapokea kutoka sehemu mbalimbali nchini na wameweza kuboresha vyumba na vifaa vya kuhudumia wagonjwa ili kuwapa matumaini mapya ya kuishi maisha ya furaha.
“leo hospitali yetu inaadhimisha siku ya figo duniani na tumewaleta wagonjwa na ndugu zao kuja kufurahi kwa pamoja na kuwapa faraha mpya katika maisha kwamba wanaweza kuendelea kuwa na maisha ya furaha,” alisisitiza Dkt Jafferji
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa hospitali hiyo, Bi Parul Chhaya alifafanua kwamba ugonjwa wa figo unahitaji nguvu ya pamoja kati ya hospitali binafsi na serikali katika kupambana nao.
“Kwa sasa tuna wagonjwa 72 wa figo kwenye hospitali yetu na tunaendelea kupokea wengine na kwetu sisi huduma kwanza na si pesa mbele katika harakati za kuokoa maisha ya watanzania wenzetu,” alisema Bi Chhaya.
Naye Meja Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambaye ni mgonjwa wa figo, Sauka Nguluo Kullaya aliongeza kwamba ni muhimu kwa serikali kuongeza vituo maalum kwenye hospitali za mikoani na wilayani ili wagonjwa wa pembezoni waanze kupata
No comments:
Post a Comment