MEYA WA ILALA AWAPA SOMO VIONGOZI SERIKALI YA MTAA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, March 10, 2018

MEYA WA ILALA AWAPA SOMO VIONGOZI SERIKALI YA MTAA




Mstaiki Meya wa Ilala  Charles Kuyeko amewataka watendaji wa serikali za mtaa kuhakikisha wanatoa huduma stahili kwa wananchi bila kudai wala kutaka rushwa yoyote badala yake wapokee kero zao na kuzitekeleza kikamilifu.

Meya kuyeko amesema hayo leo alipokuwa anazindua ofisi ya serikali ya mtaa wa Mtakuja kata ya Vingunguti jijini Dar es Salaam na kuwataka viongozi kuwahudumia wananchi kikamiifu ,pia amewataka viongozi hao  kuchukua kero zote za wananchi na kuzifanyia kazi na zile watakazoshindwa wanapaswa kuzifikisha sehemu husika ili ziweze kupatiwa majibu.

Aidha amesema katika manispaa hiyo wanampango wa  kujenga ofisi katika kila mtaa,ambapo mitaa 159 kwenye wilaya hiyo watajenga ofisi lengo likiwa ni kuhakikisha kila mtaa unakuwa na ofisi inayolingana na hadhi ya mtaa wake.

"Lengo letu ni kuhakikisha katika halmashauri ya maspaa ya Ilala tunajenga ofisi za serikali za mtaa kwa kila  mtaa inayoendana nahadhi ya huo mtaa ikiwa na lengo la kuhakikisha wananchi wanapata hudumailiyo bora zaidi" Amesema Mhe.Kuyeko.

Pia amesema atafanyia kazi changamoto zilizopo katika ofisi hiyo ilihali imejegwa na kuahidi kuzitatua ambapo changamoto hizo ni thamani za ndani ya ofisi hiyo.

Kwa upande wake naibu Meya wa Ilala Omry Kumbilamoto amesema wanamshukuru mkurugenzi wa masispaa hiyo kwa kuweza kufanikisha jambo hilo na wameweza kujenga ofisi ya kata ambapo hapo awali kulikuwa hamna ofisi na ilikuwa changamoto kubwa .

Amesema ofisi hiyo imejengwa kwa takribani sh. million 49, ambapo itahudumia wananchi 14,429 ,kwani ilikuwa changamoto ya ofisi katika mtaa huo na kusababaisha kutokuwa na usiri wa masuala yao wanayofika kuwasilisha katika ofisi hizo.

"Zamani ofisi yetu ilikuwa chakavu sana kwani ilikuwa haina usiri, wananchi akija na tatizo lake anashindwa kulieleza kwa usahihi kutokana na hali ya mazingira iliyokuwepo ,mwananchi akija ofisini atamkuta wajumbe,mwenyekiti pamoja na mtendaji wamekaa sehemu moja jambo ambalo lilikuwa changamoto kubwa katika mtaa huu"Amesema Naibu Meya .

Naye Mwenyekiti wa mtaa wa mtakuja Sharifu Mbulu, amesema anawashukuru vingozi wote walioweza kufanikisha kukamilika kwa ofisi hiyo ambapo kupitia kukarabatiwa kwa ofisi hiyo  watahakikisha wanafanya  kazi kwa weledi mkubwa.

" Nawahakikishia wananchi kupata huduma bora na nzuri kwa wakati wote wanapohitaji huduma katika ofisi za serikali wa mtaa huo wasisite kuja kwani huduma zitazidi kuwa bora"

Sambamaba na hayo ameiomba serikali kuweza kuwaboreshea miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafiri kwa wananchi na upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa haraka na uhakika zaidi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages