WANAWAKE WATUMIA MASHIRIKA KUPIGANIA 50 KWA 50 KWA KATIKA NAFASI ZA UAMUZI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, March 10, 2018

WANAWAKE WATUMIA MASHIRIKA KUPIGANIA 50 KWA 50 KWA KATIKA NAFASI ZA UAMUZI


MASHIRIKA mbalimbali nchini yametumia maadhimisho ya Siku ya Wanawake kuungana kujadili nafsi ya mwanamke kwa lengo la kuleta matokeo chanya hasa yanayohusu usawa wa asilimia 50 kwa 50 katika nafsi za uamuzi huku wakijadili kwa kina namna ya kuondoa changamoto zinazowakabili wanawake.

Baadhi ya mashirika hayo ni Shirika la Umoja wa Ulaya (EU),  Save the Children, Plan International Organization, Femina Hip, Allience Francaise na Usawa Tanzania ambapo leo wamekutaja jijini Dar es Salaam kujadili mambo yanayohusu wanawake ikiwa ni moja ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka.

Akizungumza wakati maadhimisho hayo, Mwakilishi wa Balozi wa Ufaransa nchini amesema Tanzania imepiga hatua katika kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia  na amehaidi kuwa bega kwa bega kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa mtoto wa kike.

Kwa upande wake Mwanasaikolojia na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk.Chris Mauki, amefafanua kukutana kwa mashirika hayo pamoja na mambo mengi wamelenga kuwapongeza wanawake wote walio katika sekta mbalimbali hasa katika kuleta maendeleo katika jamii.


Wakati maadhimisho, mashirika hayo yamejadilia mambo kadhaa likiwamo la kuangalia nafasi ya mwanamke katika kupewa kipaumbele ambapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema suala la kuwaweka wanawake mbele halina mjadala.

Amefafanua ni kwasababu wanawake wamekuwa bora kuliko wanaume hasa kwenye masuala ya kufikiri na kutekeleza majukumu yao kwenye jamii na kutumia maadhimisho hayo kuwatakia mafanikio mema wanawake wote katika kutelekeza majukumu yao huku akielezea huu si wakati wa kuendelea kufanya unyanyasaji kwa wanawake.

“Kutoa kipaumbele kwa wanawake halihitaji mjadala kwani wamekuwa bora katika maeneo yao ya kazi kuliko ambavyo wamekuwa wanaume walio wengi.Wamekuwa ni watu wakufikiria katika mtazamo chanya wanapotekeleza majukumu yao,"amesema Polepole.

Amependekeza mbinu za kumkomboa mtoto wa kike  na baadhi ya mbinu hizo ni kumpatia elimu mtoto wa kike ambayo itamkomboa na kutoruhusu mtu yeyote kutocheza na mtoto wa shule kwa namna yoyote.


Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Children Dignity Forum (CDF), Koshuma Mtengeti amesema ukatili kwa mtoto wa kike kwa sehemu kubwa umekuwa ukifanyika majumbani na kuomba watumie nafasi hiyo kujikita kuangalia namna bora za kuondoa changamoto zinazomkabili mtoto wa kike nchini.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages