WATOTO WALIOTELEKEZWA SASA KUPATIWA BIMA YA AFYA INAYOLIPIWA NA RC MAKONDA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, April 12, 2018

WATOTO WALIOTELEKEZWA SASA KUPATIWA BIMA YA AFYA INAYOLIPIWA NA RC MAKONDA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Mhe. Paul Makonda  amesema kinamama wote waliofika ofisini kwake wakiwa na watoto kwaajili ya kupatiwa  msaada wa kisheria baada ya kutelekezwa atawapatia  kadi za Bima ya Afya  (Toto Afya Card) Bure kwaajili ya  matibabu  ya watoto wao.

RC Makonda  amesema kadi hizo zitatolewa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 17  kwa kila mama aliefika ofisini kwake  pasipokujali idadi ya watoto alionao.


Uamuzi huo umekuja baada ya  RC Makonda  kujionea  mateso  wanayopata kinamama hao ikiwemo  watoto kuugua Magonjwa yanayohitaji garama kubwa za matibabu  na kwakuwa wengi wa kinamama hao wana  hali ngumu kimaisha wanashindwa kumudu garama na kusababisha  maumivu na mateso kwa mtoto .

Aidha  RC Makonda ,  amesema hadi kufikia mchana wa leo zaidi ya  kinamama 1,030  walikuwa tayari wamesikilizwa na Kati ya hao  watu mashuhuri 107 wakiwemo wanasiasa na viongozi wa dini  wametuhumiwa kutelekeza watoto.

Hata hivyo  Makonda , amesema kuanzia  wiki ijayo kinababa waliotelekeza watoto wataitwa ofisini kwake  kwaajili ya kutoa ufafanuzi na atakaekaidi kufika atachukuliwa  hatua kaliza kisheria.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages