NDOA YA YNA WA THE PROMISE YAZIDI KUWA MFANO UFILIPINO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, May 31, 2018

NDOA YA YNA WA THE PROMISE YAZIDI KUWA MFANO UFILIPINO

Ndoa ya mwanadada anayetajwa kuwa mrembo haswa miongoni mwa waigizaji nchini Ufilipino Kristine Hermosa Sotto ambaye ni mke wa Oyo Sotto ambaye pia ni mwigizaji, inazidi kuwa mfano wa kuigwa kwa waigizaji wengine nchini humo.

Kristine na mumewe Oyo Sotto

Kristine ambaye anafahamika zaidi kwa majina yake aliyotumia katika uigizaji kama Yna, Ara na mengineyo, yeye na mumewe wamekuwa mfano wa kuigwa kwa kumtanguliza Mungu katika kila jambo wanalolifanya hususani katika ndoa yao. Yna amekuwa akitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuweka vifungu mbalimbali vya Biblia na picha zake chache, lakini pia akimshukuru Mungu kwakila jambo analopitia.

Wawili hao ambao kwasasa wamejaliwa watoto wanne kati yao akiwemo waliyemchukua kumlea kutoka kituo cha yatima, wamekuwa mstari wa mbele katika kuwalea watoto wao kwenye misingi bora, ikiwa pamoja na kutakiana heri kwa kunukuu vifungu vya Biblia kama ilivyokuwa siku ya wanawake duniani ambapo Oyo akaamua kuchukua ujumbe kutoka kitabu cha Mithali 31:10, 31:28-31 ujumbe ambao ulipokelewa vyema na mashabiki wao kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.


Kristine na Oyo ambao wamewahi kuigiza pamoja katika tamthilia iliyowahi kuonyeshwa na TBC enzi hizo TVT iitwayo Prinsensa Ngi Banyera (Princess of Fish pot) Kristine akiitwa Maningning na Oyo akiigiza kama mwanasheria kwa jina la Victor Abad, wote kwa pamoja wamesimama ugizaji toka waoane, nasasa wamejikita kwenye masuala ya biashara ambapo wamefungua duka la kuuza baiskeli linaloitwa Konabikes pamoja mgahawa uitwao Kscafe.

Kristine na familia yake

Hata hivyo mwaka jana walishiriki kwenye igizo la vichekesho liitwalo Hay Bahay ambao wameigiza pamoja na baba mzazi wa Oyo aitwaye Vic Sotto katika runinga ya GMA ambayo ni runinga pinzani na ABS-CBN ambao ndio wanaoongoza kwa kuuza maigizo maarufu likiwemo Pangako Sayo ndani na nje ya nchi hiyo.

Kristine alifanikiwa kujitangaza vyema kwenye fani ya uigizaji pale alipoigiza tamthilia ya Pangako Sa’yo au The Promise kwakutumia jina la Yna Macspac na kijana Jericho Rosales almaarufu kama Angelo ambaye naye kwasasa ameoa mwanamitindo aitwaye Kim Jones huku tayari akiwa na mtoto mkubwa wa kiume mwenye miaka 18 aitwaye Santino Rosales aliyempata enzi za The promise ikiwa maarufu sana nchini humo na mwanamke aliyekuja kumtambulisha hadharani hivi karibuni.

Jericho akiwa na mwanaye Santino
Jericho akiwa na mkewe Kim, siku ya ndoa yao

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages