TEACHERS JUNCTION YAWANG'ARISHA KWA KUWAPA TUZO WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, May 30, 2018

TEACHERS JUNCTION YAWANG'ARISHA KWA KUWAPA TUZO WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI

Jumla ya  shule 45 kutoka katika mikoa 13 nchini zikiwemo za Serikali ambazo nazo zimefanya vizuri katika mtihani wa Darasa la Nne na la Sita.

Akiongea wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza na kuwapa zawadi baadhi ya watoto waliojitokeza kuhudhuria katika hafrl hiyo, Hafisa Miradi wa Taasisi ya Teachers Junctions Njama Salim amesema Mradi huu ulianzishwa Mwaka 2017 chini ya Usimamizi wa Taasisi hiyo ikiwa na lengo la kuimarisha upimaji wa wanafunzi kwa upande wa Shule za Msingi za watu binafsi pamoja na zile za serikali.

Amesema katika Mashindano ha shule ya Ubungo ya Tigohane imeibuka kidedea kwa kuchukua ushindi wa jumla kwa Mtihani wa darasa la Nne na kuongeza kuwa Watoto wote walioshiriki Mtihani huo walikua katika Mchuano mkali.

Amesema Lengo Kubwa la Mtihani huo ni kuisaidia Serikali katika kuwapima wanafunzi na kwamba kwa mara ya kwanza wameweza kupata ushiriki mzuri kutoka katika shule za Serikali zinazotumia Mtaala wa kingereza.

Upande wake Msemaji kutoka shule ya wavulana ya Sullivan Provost kwa niaba ya Mkuu wa shule Felix Kavishe, amesema kuwa wataendelea kuunga mkono mashindano hayo kwani yanaleta chachu ya ufaulu. 

Mradi wa INTERSCHOOL EXAMS AND CONSULTANCY ni Mradi wa miaka Mitatu na unalenga katika kutoa ushauri na kuhamasisha wanafunzi kwa kuwapatia Zawadi mbalimbali hasa wale wenye wastani Mkubwa.

Baadhi ya wanafunzi waliohudhulia hafla hiyo na baadhi yao wameibuka washindi katika mitihani yao ambayo, katika mashindano hayo Shule 45 zimeshiriki mashindano hayo.
Mwanafuzi wa Darasa la nne katika Shule ya Msingi ya Junior iliyoko Mzumbe Morogoro Jackline Bahasha, akivalishwa Medali ya ufahulu wa jumla na Meneja wa Mauzo na Masoko wa New Habari 2006, Mrs Rehema Ahmed.
Mwanafunzi wa Darasa la nne katika Shule ya Msingi ya Diamond iliyoko  Dar es Salaam Abdusalaam Selemani, akivalishwa Medali ya ufahulu wa jumla na Meneja wa Mauzo na Masoko wa New Habari 2006, Mrs Rehema Ahmed.
Mwanafunzi wa Darasa la nne katika Shule ya Msingi ya Tigohane iliyoko Wilaya ya Ilala Dar es Salaam  Brian Richard, akipokea Ngao ya ushindi kwa kuongoza kwa masomo yote katika shule zilizoshindanishwa na Meneja wa Mauzo na Masoko wa New Habari 2006, Mrs Rehema Ahmed.
Mwanafunzi wa Darasa la sita katika Shule ya Msingi ya Dominic Savio ya Iringa, Gloria Castro, akipokea Ngao ya ushindi kwa kuongoza kwa masomo yote katika shule zilizoshindanishwa katika masomo ya darasa la sita na Meneja wa Mauzo na Masoko wa New Habari 2006, Mrs Rehema Ahmed. Mashindano hayo yalioanzishwa na Mradi wa  Teachers Junction.
Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari ya wavulana Sullivan Provost, Felix Kavishe akizungumza na walimu wazazi pamoja na wanafunzi kwaniaba ya Mkuu wa shule hiyo Mr Alex Nichoraus wakati wa sherehe za kutoa tuzo kwa wanafunzi wa Darasa la sita na lanne waliofanya vizuri ikiwa shule ya Sullivan ilikuwa wadhamini wakuu ambapo waliandaa Ngao kwaajili ya darasa la sita katika mashindano hayo Shule 45 walishiriki  hayo yalioanzishwa na Mradi wa  Teachers Junction.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wavulana Sullivan Provost, akitoa neno kwa wanafunzi waliohudhuria mashindano hayo nakuwasihi kama wakitaka kuendelea vizuri na ufaulu wao basi wachague shule ya Sullivan kwaajili ya kupata elimu bora mashindano hayo yalioanzishwa na Mradi wa  Teachers Junction.
Afisa Mradi wa Teachers Juction Njama Salum akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo shule 45 walishiriki mashindano hayo.
Mkuu wa Shule ya Msingi Tigohane iliyoko Wilaya ia Ilala Dar es Salaam Meleck Macha alielala chini, akibubujikwa na machozi baada yakutangazwa kuwa Mwanafunzi wa  shule yake Brian Msangi,  ameibuka kidedea na kujinyakulia Ngao ya ufahulu katika mitihani yote kwa darasa la nne, Shule 45 zimeshiriki mashindano hayo.
Mkuu wa Shule ya Msingi ya Dominic Savio Sister Beatrice Kapinga, Iringa, akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Shule ya Sekondari ya wavulana Sullivan Provost, kwakuona umuhimu wa mashindano hayo na kuandaa ngao hiyo kwa wanafunzi wa darasa la sita ambayo shule ya Dominic Savio ndio imenyakua ngao hiyo kupitia mwanafunzi wake Gloria Castro ameibuka kidedea na kujinyakulia Ngao ya ufahulu katika mitihani yote kwa darasa la sita, ambapo Shule 45 kutoka mikoa 13 nchini.


MATUKIO KATIKA PICHA







Wanafunzi wa Shule ya Wavulana na Sullivan wakiwa katika hafla hiyo.































No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages