Rais
wa Zanzibar wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dk. Ali Mohammed Shein (wa pili kushoto), akiagana na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Theobald Sabi katika hafla ya futari
iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake mjini Zanzibari hivi
karibuni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji NBC Bw.Theobald Sabi wakati alipofika Zanzibar Beach Resort jana katika Futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC hapa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akichukua chakula cha futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC hapa Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort (kulia) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid.
Baadhi ya Viongozi mbali mbali wakichukua chakula cha futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC hapa Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Baadhi ya Wateja wa Benki ya NBC hapa Zanzibar walioalikwa katika futari iliyoandaliwa jana katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha na Uongozi wa Benki ya NBC mara baada ya Futari waliyoiandaa jana katika
Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, akiwepo na
Mkurugenzi wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein (wa tano kushoto)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akiagana na Viongozi wa Benki ya NBC mara baada ya Futari waliyoiandaa katika
Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, hafla iliyohudhuriwa na Viongozi mbali mbali na Wananchi.
Rais wa Zanzibar wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein ameipongeza Benki ya NBC kutokana na kasi
yake na juhudi za kukuza uchumi wa Zanzibar.
Akizungumza kwa niaba ya rais wa Zanzibar katika hafla ya futari
iliyoandaliwa na benki hiyo iliyofanyika mjini Zanzbar hivi karibuni, Mkuu wa
Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud amesema pato la taifa limekuwa
likikuwa mwaka hadi mwaka kutokana na mchango unaotolewa na taasisi mbali mbali
ikiwemo Benki ya NBC.
Aidha Dk.Shein ameihimiza benki hiyo kuendelea na juhudi zake za
kuimarisha mazingira bora na huduma kwa wateja wake ili kwenda sambamba na kasi
ya mabadiliko ya huduma za kifedha yanayotokea siku hadi siku na kukuza
maendeleo bora nchini.
Hata hivyo ameipongeza Benki hiyo kwa kuonesha umuhimu kwa
wateja wake kwa kurejesha miongoni mwa faida wanazozipata ikiwemo kwa njia hiyo
ya kufutarisha na kutoa huduma nyengine mbali mbali kwa jamii.
Awali akizungumza katika hafla hiyo ya futari Kaimu Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBC, Dk. Kassim
Hussein amesema kukuwa kwa huduma za kifedha Zanzibar pia kunatokana na huduma
bora zinazotolewa na benki hiyo inayokwenda sambamba na mahitaji ya wateja
wake.
Amesema mazingira salama yaliopo Zanzibar yanayoimarishwa na
viongozi wakuu wa nchi imewezasha benki hiyo kufanya kazi zake za kutoa huduma
za kifedha kwa ufanisi na umakini Zaidi.
No comments:
Post a Comment