Kampuni ya Uber imewekeza katika teknolojia ambayo imeiwezesha kuweka mkazo mkubwa kwenye usalama wa wasafiri na madereva kuanzia mwanzoni mwa safari hadi mwisho: kabla ya msafiri kuabiri gari, wakati wote wa safari na baada ya kufika mahali anakoenda. Kuanzia pale dereva anapoandikishwa kwenye mfumo, madereva wote washirika wanatakiwa kutimiza vigezo muhimu vya kiusalama sambamba na magari wanayotumia. Kampuni ya Uber pia inatoa msaada wa usalama kwa madereva kupitia Timu yake ya Kushughulikia Matukio mbalimbali inayofanya kazi usiku na mchana. Kampuni ina mpango endelevu wa kuendesha semina elekezi za kuwapa madereva washirika mafunzo muhimu yanayohusu usalama.
Masharti ya Kujiandikisha jijini Dar es Salaam
· Masharti ya kuwa Dereva:
o Leseni ya Dereva (Daraja la C, C1, C2, C3): Madereva wote wanaotumia app ya Uber wanatakiwa wasajili magari yao kwa shughuli za biashara na wawe na leseni ya biashara.
o Uchunguzi wa tabia ya dereva: Madereva wote hufanyiwa uchunguzi wa kina ili kujiridhisha na tabia na mienendo yao kubaini iwapo inaendana na masharti ya kutumia app ya Uber. Uchunguzi huu unajumuisha kupata stakabadhi ya jeshi la polisi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.
o Vikao vya mafunzo maalum: Vikao hivi vinahusu kusoma kozi fupi kwenye Kituo cha Dereva wa Uber, baada ya kufaulu, akaunti ya dereva itafunguliwa na baadaye anaweza kutumia app ya Uber. Madereva wanatakiwa kuhudhuria vikao vya mafunzo maalum, ambapo wafanyikazi wa Uber watawaelekeza kuhusu namna wanaweza kutoa huduma zinazotosheleza mahitaji ya wasafiri. Vikao hivi pia hutumika kufafanua Miongozo ya Jumuiya ya Uber, ambayo inaeleza waziwazi viwango vya ubora ambavyo kampuni ya Uber imeweka sambamba na kuanisha tabia na mienendo ambayo haikubaliki na sera ya Uber mtu anapotumia app hii na adhabu ya kufungiwa akaunti ya Uber kwa msafiri au dereva yeyote atakayeenda kinyume na miongozo hii.
· Gari:
o Kadi ya Gari Lililosajiliwa kwa Shughuli za Biashara: Magari yote yanatakiwa yawe na kadi ya gari inayoonesha kwamba gari limesajiliwa kufanya shughuli za biashara kutoka kwa Mamlaka ya Mapato (TRA)
o Bima: Magari yote yanayotumia Uber lazima yawe na bima ya magari ya biashara na bima ya kinga ya umma.
o Kibandiko cha kuendeshea: Maderewa wanaotumia Uber jijini Dar es Salaam wanatakiwa walipie kibandiko kinachotolewa na Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kitakachosaidia maafisa wa halmashauri kuwatambua madereva washirika wa Uber.
· Usaidizi kwa Madereva washirika:
o IRT: Timu yetu ya Kushughulikia Matukio (IRT) inapatikana usiku na mchana, siku 7 za wiki kwa ajili ya kushughulikia matukio au ajali yoyote punde tu inapotokea kote ulimwenguni.
o Namba za simu za dharura: Kampuni ya Uber imeingia ubia na kampuni ya Ulinzi ya SGA Security, kampuni ya humu nchini ili kuwapa madereva namba maalum za simu wanazoweza kutumia kuwasiliana kunapotokea dharura yoyote ya kiusalama.
No comments:
Post a Comment