Dar es Salaam, 9-Julai 2018 – Benki ya KCB Tanzania imefanya uzinduzi wa tawi lake la 14 lililopo Mbagala jijini Dar es salaam. Tawi hilo limezinduliwa rasmi na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dr. Ashatu Kijaji ambaye aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mh, Felix Lyaniva, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke- Mh. Abdallah Chaurembo, Ndugu Mbunge wa Temeke – Mh Issa Mangungu, Ndugu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke- ACP Emmanuel Lukula, Ndugu Diwani wa kata ya Mbagala- Jumanne Kambangwa, Ndugu Viongozi na maafisa mbalimbali wa Serikali, Wakurugenzi pamoja na wafanyakazi wa KCB Bank.
Katika uzinduzi huu wazungumzaji Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi.Walitoa mafanikio machache ambayo KCB imeweza kufanya kwa jamii.
KCB Bank imewezesha miradi mikubwa ya maendeleo ya nchi yetu kutokana na rasilimali za KCB Group (strong balance sheet). Miradi hiyo ni kama Barabara ya Msata hadi Bagamoyo, Ujenzi wa Terminal Three (3) JNIA, jengo la One stop Centre TPA na Emergency Laboratory Building (Ofisi ya Raisi, Makumbusho) kwa kutaja tu michache.
Katika hotuba yake mwenyekiti alisema, “Ndugu mgeni rasmi natumaini unakumbuka vizuri mwaka 2017 uliitikia wito wa kuwa mgeni rasmi kwenye warsha ya 2jiajiri iliyokutanisha wanawake zaidi ya 1500 hapa jijini Dar es salaam. Leo nina furaha kurudisha mrejesho kuwa baada ya kutambua mahitaji ya kifedha ya wanawake wajasiriamali, KCB Banki imeshazindua “2jiajiri Women Account” amabayo inawawezesha kuweka akiba na kupata mikopo kwa masharti mepesi na rafiki. Ulitupa changagmoto nasi tukaifanyia kazi.”
Wazungumzaji walisisitizakuwa Tawi hili la Mbagala ni sehemu ya jitihada za kuweza kufikia wateja wao wengi lakini pia kutanua wigo wa huduma za kibenki. Waliendelea kwa kusisitiza kuwa Mbagala ni moja ya maeneo yenye idadi kubwa ya watu jijini Dsm vilevile kuna uwepo wa biashara ndogo, za kati na zile kubwa ambazo zinajumuishwa viwanda, usafirishaji, elimu na kadhalika. Wanaamini kuwa tawi hili litakidhi mahitaji ya kifedha kwa wateja wao wote katika eneo hilo na maeneo ya jirani.
Wazungumzaji waliwakaribishawakazi wote wa Mbagala na wakaribu kutumia huduma zao za kibenki na kufahamu zaidi faida zitokanazo na kuwa mteja wa KCB Bank ikiwemo mikopo, akaunti za akiba zenye faida lukuki, mtandao mkubwa wa ATM zaidi ya 962 Afrika mashariki.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa KCB Bank Bw. Cosmas Kimarioalisema benki hiyo inaunga mkono jitihada za serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi kwa kuboresha huduma zetu ili kuendana na kasi ya mabadiliko na ukuaji wa uchumi.
Vilevile Mkurugenzi Mtendaji aliendelea kusema, kipindi cha kota ya kwanza ya 2018 benki hiyo imeweza kupata faida ya shilingi Bilion 3.6/- benki imeweza kuthibiti madeni chechefu (NPL) kufikia asilimia 7% kiwango ambacho ni kizuri katika utendaji wa kibenki.
Walimaliza kwa kusisitiza kuwa KCB Bankwataendelea kuboresha huduma na kuzisogeza karibu na wateja wao kwa kupitia njia za kidigitali kama vile simu za mkononi, mtandao wa intaneti pamoja na mawakala. Wanaamini kuwa uboreshaji huu sio tu utarahisisha upatikanaji wa huduma zao bali pia utaongeza idadi ya wananchi wanaofikiwa na huduma za kifedha (financial inclusion).
Kuhusu Benki ya KCB
Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 250, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 12,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki katika Afrika Mashariki. Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda.
KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation.
Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba ,Buguruni, Oysterbay, Pugu jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro.
Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment