Na Said Mwishehe, Dar es Salaam
RAIS Dk.John Magufuli amewataka watalaam nchini kuwa wazalendo kwa nchi yao huku akieleza kuwa baadhi ya watalaam ndio chanzo cha kukwamisha miradi na hasa ya maendeleo.
Pia ametoa onyo kwa wataalam wa mazingira ambao wametoa mapendekezo ambayo ameyaita ua hovyo na yenye lengo la kukwamisha mradi wa umeme wa maji wa Stiglers georg na amewataka kuyafuta mapendekezo yao mara moja na ole wao wakishindwa kuyabadilisha.
Rais Magufuli amesema hayo wakati anazindua rasmi flyover ya Mfugale katika makutano ya Tazara jijini Dar es Salaam ambapo ametumia nafasi kueleza namna ambavyo baadhi ya watalaam nchini wamekuwa chanzo cha kukwamisha miradi."Ngoja nitoe mfano mmoja tu wa namna ambavyo baadhi ya watalaam wetu wanakwamisha miradi yenye tija kwa watanzania."Tena ni wataalam ambao wamezaliwa Tanzania na wamesomeshwa na Serikali,wengine ni weusi kuliko hata mimi lakini wanafanya maamuzi ya hovyo kabisa.
"Tunafahamu umeme wa maji ndio wenye bei nafuu kabisa kuliko umeme wowote. Mkakati wa Serikali ni kuhakikisha tunapata umeme wa maji kupitia mradi wa Stiegler's Gorge,"amesema. Ameongeza wakati Serikali inataka kuanza ujenzi huo na fedha zipo tayari lakini watalaam wa mazingira wametoa mapendekezo yao.
"Ukiisoma ile ripoti yao utakutana na mapendekezo mengi na baadhi ya mapendekezo yanasema watakaokuwa wanajenga eneo hilo wasijisaidie eneo hilo, waende umbali wa kilometa 10." Pendekezo lingine chochote ambacho kitapelekwa hapo kipimwe kwanza,yaani kama unataka kupeleka mchicha kwa ajili ya watu waliopo eneo la mradi basi lazima upimwe. Chochote ambacho utakipeleka eti wanataka kipimwe.
Pia kuna pendekezo la kwamba ikitokea gari ambayo ipo kwenye eneo la mradi ikiharibika haitakiwi kutengenezwa hapo, yaani hata kubadilisha mafuta, kisa hawataki yamwagikie eneo hilo. Haya ni mapendekezo ya kijinga,"amesema Rais Magufuli.
Ameongeza kuwa ukiangalia mapendekezo hayo unapata picha kwamba hawataki mredi huo utekelezwe na wanaoshiriki kuweka mazingira hayo ni baadhi ya watalaam ambao wanaendekeza maslahi binafsi. Sasa niwahakikishie mradi huo utajengwa ili kupunguza bei ya umeme ambayo ni kubwa.Hatuwezo kushindana katika viwanda wakati umeme weti bei iko juu.
"Hivyo nimewaagiza hao watalaam wa mazingira kubadilisha mapendekezo hayo na ole wale huyo mtaalam asipoyabadili," amesema Rais Magufuli.Akifafanua muhusu bei ya umeme amesema uniti moja ya umeme nchini Marekani ni Senti 0.12, Uingereza uniti moja ni senti 0.15 lakini hapa nchini Unit moja ya umeme ni Senti 10.7. Amefafanua mkakati wa Serikali ni kuwapunguzia gharama ya bei ya umeme na hilo halitabadilika,hivyo amewataka watalaam kuwa wazalendo badala kusikiliza watu kutoka nje.
Amesema kumewepo na changamoto kubwa hasa unapotaka kukopa fedha kwa ajili ya kufanya maendeleo na unaweza kuomba na usipate fedha lakini ukitaka mkopo kwa ajili ya mambo ambayo hayana tija kwa wananchi unaupata haraka." Sasa tunazo fedha za kufanikisha mradi huo lakini watu wanakwamisha.Watalaam wetu igeni utumishi wa kizalendo na wa kutukuka kama Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale," amesema Rais Magufuli.
No comments:
Post a Comment