Mkurugenzi
Idara Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika (CBA) Julius
Konyani (kushoto), akimkabidhi Mshindi
wa Bajaji katika promosheni ya Shinda na M-PAWA Bi.Mariam Balawa
mkazi wa Kibamba jijini Dar es Salaam, ambapo washindi watano walikabidhiwa
bajaji zao na Bi Sophia mkazi wa Bukoba amekabidhiwa kitita cha Shilingi
milioni kumi, hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Benki
hiyo Kijitonyama anaeshuhudia (kulia) ni
Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya.
Meneja Masoko wa Vodacom,
Noel Mazoya (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla
yakuwakabidhi washindi wa Bajaji katika promosheni ya Shinda na M-PAWA ambapo
washindi watano walikabidhiwa bajaji zao na Bi Sophia mkazi wa Bukoba
amekabidhiwa kitita cha Shilingi milioni kumi, hafla ya makabidhiano hayo
yamefanyika kwenye viwanja vya Benki hiyo Kijitonyama, (katikati) ni Mkurugenzi Idara Wateja binafsi na
Masoko wa Benki ya Biashara Afrika (CBA) Julius Konyani na kulia ni Meneja
Biashara Huduma yaM-PAWA Gloria Njiu.
Mkurugenzi
Idara Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika (CBA) Julius
Konyani (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla
yakuwakabidhi washindi wa Bajaji katika promosheni ya Shinda na M-PAWA ambapo
washindi watano walikabidhiwa bajaji zao na Bi Sophia mkazi wa Bukoba
amekabidhiwa kitita cha Shilingi milioni kumi, hafla ya makabidhiano hayo
yamefanyika kwenye viwanja vya Benki hiyo Kijitonyama, (kushoto) ni Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya na
kulia ni Meneja Biashara Huduma ya M-PAWA Gloria Njiu.
Benki ya CBA na Vodacom imekabidhi zawadi kwa
washindi wake wa promosheni ya SHINDA NA M-PAWA leo katika tawi la benki hiyo
lililopo Kijitonyama.Zawadi hizo ni bajaji tano mpya. Promosheni hiyo iliyodumu
wa wiki 6 ilifikia tamati hapo tarehe 14 mwezi huu.
Mshindi wa milioni kumi ni Mama Sophia Sarapion
(54) ni mwenyeji wa Bukoba ambapo anaishi akijushughulisha na shughuli ya
kilimo cha mihogo, Benki imepanga kumtembelea mshindi huyo mwezi ujao. Washindi
watano wa bajaji ambao ni AbeidAbeid, Lucas Ngoye, MariamuBarawa, Hassan
MsabilanaHamisiMpela wanatokea maeneo tofauti tofauti ya Tanzania ambayo ni
Arusha (1),Chalinze (1) Dar Es Salaam (3).
Mama Sophia ambaye amefurahi sana ameishukuru
benki ya CBA na Vodacom kwa kuunda promosheni hii akisema “M-Pawa haijanisaidia
tu kwenye maisha yangu ya kila siku linapokuja swala la kutunza akiba na kupata
mikopo inayoniwezesha kufanikisha mipango yangu bali imebadilisha maisha yangu
kabisa.Nitatumia fedha hizi vizuri
katika kuboresha shughuli yangu ya kilimo”
Washindi watano wa bajaji wakiwa wamefurahia
sana ushindi huo wameisifia benki ya CBA na Vodacom kwa mkakati wao wa
kuirejeshea jamii fadhila kwa njia ya kuwezesha wananchi huku wakiwataka wateja
wa M-Pawa kuendelea kutumia M-Pawa na kuwakaribisha ambao bado hawajaanza
kutumia kujiunga.
Akizungumza kwenye sherehe hiyo ya makabidhiano
ya zawadi hizi kwa washindi,Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa benki ya CBA Bwana
Julius Konyani alieleza “Promosheni ya SHINDA NA M-PAWA
ililenga kuwafikia wananchi wasiofikiwa na huduma za kibenki na kuwawekea
mazingira ya kujiwekea akiba huku ikiwapa changamoto ya kurudisha mikopo yao
kwa wakati pale wanapokuwa wamechukua mkopo.Mikopo yetu ina riba ndogo sana
kwani lengo letu hasa ni kuwawezesha kiuchumi wateja wetu.Lengo letu jingine
ilikuwa kuwashukuru na kuwazawaida wateja wetu msimu huu wa sikukuu.Tunafurahi
washindi wetu wameweza kuwa ishara ya mafanikio yetu katika lengo hili
Benki ya CBA kwa ushirikiano na Vodacom tutaendelea kutoa
huduma hii ya Mpawa kuweza kuwafikia watanzania wengi zaidi, wakiwemo wakulima
na wajasiriamali kuweza kuwakwamua kwa kuwapa mikopo midogo midogo ya mpaka
shilingi laki tano. Mbali na hayo M-Pawa inawapa fursa wateja kuhifadhi hela
zao kwa malengo yao ya baadae, akiba yako ndio Malengo yako. Katika kipindi hichi cha promosheni tumefanikiwa kuwapata wateja wapya zaidi ya milioni moja wa M-pawa,
hivyo Mpawa imekuwa na jumla ya watumiaji wa huduma hii wanayokaribia milioni
nane.
Nawapongeza sana
washindi wetu wote zaidi ya 1200 na pongezi za kipekee kwa mshindi mkuu na
washindi watano waliojishindia bajaji wakawe mabalozi wetu popote watakapopita
na waendelee kuhamasisha matumizi ya Mpawa.”
Kampeni ya SHINDA NA M-PAWA ilifanyika kwa muda wa wiki 6
kuanzia tarehe 8 Novemba hadi tarehe 13 Desemba ikilenga watumiaji wa huduma ya
M-Pawa.Jumla ya washindi 1,296 walipatikana katika kipindi hicho cha
promosheni.Huu ni Ushahidi kwamba jitihada za benki ya CBA na Vodacom katika
kuwafikia wananchi wasiofikiwa na huduma za kibenki zinaendelea vyema.
Commercial Bank of Africa (CBA) is a commercial bank
in Tanzania, regulated by bank of Tanzania. The bank is a subsidiary of the
Commercial Bank of Africa Group.
No comments:
Post a Comment