Washindi wa Kapu la sikukuu katika picha ya pamoja na maafisa wa MultiChoice Tanzania mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.
Baadhi ya washindi wa Kapu la sikukuu kutoka DStv wakipokea zawadi zao kutoka kwa Grace Mgaya Afisa Uhusiano MultiChoice Tanzania na Meneja Mkuu wa E Fm Radio na Tv E Mohamed Lukwili.
Afisa masoko MultiChoice Tanzania Esther Mtei (kushoto) akikabidhi zawadi kwa moja kati ya washindi wa Kapu la sikukuu Bw Mohamed kutoka Mbezi.
Afisa masoko MultiChoice Tanzania Esther Mtei (kushoto), Meneja Mkuu E Fm na Tv E Mohamed Lukwili wakimkabidhi moja kati ya washindi wa Kapu la sikukuu kutoka DStv bi. Mariam Mkwaje.
Katika kusherekea msimu huu wa sikukuu kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia kisimbusi chake maarufu cha DStv imemwaga zawadi za makapu ya sikukuu kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani yaliyosheheni vyakula mbalimbali ikiwemo mchele, mafuta, sukari, na viungo mbalimbali muhimu kwa ajili ya sikukuu bila kusahahau mbuzi mzima kwa kila mshindi na zaidi visimbusi vya kisasa vya DStv vilivyounganishwa na vifurushi vya mwezi mzima wa Bomba kwa washindi wote wa shindano la ‘Kapu la Sikukuu’ lilioendeshwa mapema mwezi huu kwa kushirikiano na kituo bora cha redio cha E Fm .
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Afisa Masoko kutoka MultiChoice Tanzania Bi. Esther Mtei amesema kuwa, “Msimu huu wa sikukuu ni muda mzuri na sahihi wa kukaa nyumbani na familia na hii ndiyo sababu DStv leo tumewazawadia washindi hawa jumla ya makapu 30 ya vyakula yaliyosheheni mahitaji yote ya muhimu kwa ajili ya jikoni, mbuzi mzima kwa kila mshindi sambamba na visimbusi vya DStv kwa kila mmoja pamoja na kufungiwa bure ili kuwawezesha kusherekea sikukuu wakiwa majumbani mwao huku wakipata burudani ya kipekee kupitia vipindi bora vinavopatikana ndani ya king’amuzi cha DStv ikiwemo ligi kuu ya Uingereza (EPL) , vipindi maalum vya watoto pamoja na sinema kadha wa kadha maalum kwa ajili ya msimu huu wa sikukuu” alisema Esther.
Naye meneja mkuu wa E Fm Radio na Tv E Mohamed Lukwili alieleza kuwa,” Shindano hili liliwataka wasikilizaji wa E Fm radio kusikiliza na kufatilia vipindi tofauti kwa kipindi cha mwezi mmoja kisha kujibu maswali yaliyoulizwa ili kuweza kujishindia zawadi hii nono ya kapu la sikukuu kutoka kwa DStv”, alisema Lukwili.
Kwa upande wake bi. Mariam Mkwanje mmoja kati ya washindi wa shindano la kapu la sikukuu alisema, “Kwa niaba ya washindi wenzangu tuliofika mahali hapa asubuhi ya leo, tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa uongozi wa kampuni ya MultiChoice Tanzania pamoja na E FM radio kwa kuweza kutukumbuka katika kipindi hiki cha sikukuu, tumefurahi sana na hakika tunaahidi kuendelea kuangalia DStv pamoja na kuwa wasikilizaji wazuri wa E Fm radio.
No comments:
Post a Comment