Serikali kupitia mifuko ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi imedhamiria kuwawezesha vijana kwenye sekta ya uvuvi kwa kuwapatia mikopo ya nyenzo za uvuvi na mitaji ili Vijana wengi zaidi washiriki kwenye sekta ya uvuvi halali hali itakayopelekea ongezeko na nafasi zaidi za Ajira hususani kwa Vijana.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde wakati akiongea na Vijana katika kata za Chato kati na Muganza,Wilayani Chato,Geita ambapo Mavunde alitumia fursa hiyo kuwahamasisha Vijana kuunda Vikundi vya Uzalishaji mali ili kuwa na sifa ya kukopesheka kwa minajili ya kuongeza tija katika shughuli hizo za kiuchumi.
“Serikali itaendelea kutekeleza programu mbalimbali za uwezeshwaji kichumi na za kuongeza ujuzi ili kuwajengea uwezo Vijana wa kitanzania kuwa na ujuzi stahiki utakaowawezesha kujiajiri na kuajiri Vijana wengine”Alisema Mavunde
Akimkaribisha Naibu Waziri Mavunde,Mbunge Wa Jimbo la Chato am baye pia ni Waziri wa Nishati Mh Dr. Medrad Kalemani ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa program ya uwezeshaji Vijana kiuchumi na progamu ya Kilimo kupitia Kitalu nyumba*(Greenhouse)* ambayo Vijana wa Mkoa wa Geita watanufaika na kuahidi kuwasimamia Vijana hao katika kuunda SACCOS ili kujiongezea wigo mpana wa kuwa na fursa za kukopesheka na kuongeza mtaji katika shughuli za kiuchumi.
No comments:
Post a Comment