Baadhi ya washiriki na wadau wa
Kampeni ya Jiongeze tuwavushe salama wakiwa katika uzinduzi huo.
Na.Vero
Ignatus,Arusha.
Uzinduzi wa
kampeni ya jiongeze tuwavushe salama umefanyika mkoani Arusha ikiwa na lengo la
''Kupunguza vifo vitokananvyo na uzazi'' na kuhakikisha mama na mtoto wanakuwa
salama kabla na baada ya kujifungua.
Akizungumza
katika uzinduzi huo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa watendaji
wote wa wizara ya afya ngazi ya mkoa watende kazi kwa weledi ili waweze
kupunguza vifo vya wakina mama wakati wa kujifungua ambapo kwa ngazi ya mkoa ni
40%na Kitaifa ni 28%.
Kampeni
hiyo iliyobeba Kauli mbiu isemayo''Jiongeze Tuwavushe Salama''na Maudhui
yasemayo '' Kila mmoja wetu anao wajibu wa kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi,
maneno basi, sasa vitendo''
Amesema
kuwa kampeni hiyo ni ya muhimu kwani inakwenda sambamba na lishe kwa mama
mjamzito ili aweze kujifungua salama na mtoto atakayezaliwa awe mwenye afya
njema,''Mwanaume ni wajibu wako kutambua kuwa mwanamke anapokuwa mjamzito ndio
wakati wako wa kuwa karibu na mkeo, msindikize Kliniki, pimeni afya pamoja
leeni mimba pamoja na mtoto akizaliwa mtamfurahia''. Alisema Gambo.
Ameainisha
sababu kuu ambazo zinasababisha vifo kwa akina mama wajawazito ni pamoja na
mama kutohudhuria kliniki mapema,kutokwa damu nyingi wakati wa kujifungua na
baada ,shinikizo la damu. Amesema lishe duni imekuwa sababu kubwa ya wakina
mama kujifungua watoto njiti ambapo pia vifo vya watoto hao ni 25 kati ya kila
vizazi hai 1000husababishwa na kushindwa kupumua na wengine kuzaliwa kabla ya
wakati.
Kwa upande
wake Daktari mkuu wa mkoa Wedson Sichalwe amesema Tafiti zilizofanyika mwaka
2015/2016 zinaonyesha kiwango cha vifo vitokanavyo na uzazi ni 556 kwa kila
vizazi hai 100,000 ambayo ni sawa na vifo 11,000 kila mwaka,sawa na wanawake 30
hufariki kila siku, kutokana na matatizo yatokanayo na uzazi.
Dkt.
Sichalwe ameainisha kuwa changamoto kubwa waliyonayo ni ukosefu wa dawa
lishe,ukosefu wa virutubisho ambavyo hupelekea matatizo kwa mtoto akiwa tumboni
hata kuzaliwa njiti au akiwa amefariki.Dkt amesema hiyo changamoto ya lishe
katika mkoa imesababisha watoto wengine kuzaliwa wakiwa na udumavu halo
inayopelekewa kuja kuwa na taifa lenye watoto wengi wenye tatizo hilo endapo
hatua za haraka hazitachikiliwa.
Baadhi ya
washiriki na wadau wa afya akiwemo Dkt. Emmanuel Maeda amesema swala la elimu
kwa jamii ni changamoto hivyo wao wamekuja na kitu kiitwacho Vunja ukimya
kwaajili ya kumkumbusha mwanaume kutambua wajibu wake pale mke anapokuwa
mjamzito.
''Mwanamke
anapokuwa mjamzito inamuhitaji mwanaume kuelewa, anapaswa atambue mama mjamzito
anahitaji lishe bora ili ajifungue salama, ikiwa kwenda pamoja kliniki na
kutambua changamoto anazopitia na siyo wao kukaa pembeni na kusema kwani mimi
ndo nimebeba mimba''alisema Dkt. Maeda.
Nae Munga
kutoka Japayco nae alishauri kuwa kuwepo na siku ya afya vijijini ina lazima
juhudi ziongezwe kuhakikisha kuangalia zaidi mama na kichanga anavuka salama na
kila mjamzito lazima aende kliniki na hospitali kujifungua.
Kampeni ya
Jiongeze tuwavushe salama ilizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais Mhe. Samia
Suluhu Hassan 6Novemba 2018 mkoani Dodoma. ampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama
inatekelezwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
pamoja na Mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo UNICEF.
Katibu Tawala wa Jiji la Arusha
Richard Kwitega akizungumza katika Uzinduzi wa Kampeni ya Jiongeze tuwavushe
salama iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa Jijini Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo, akibadilishana jambo na Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha Dkt. Wedson
Sichalwe kwenye Kampeni ya Jiongeze tuwavushe salama.
No comments:
Post a Comment