RC MAKONDA AWAFUNDA MADIWANI WA ILALA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, April 16, 2019

RC MAKONDA AWAFUNDA MADIWANI WA ILALA


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka madiwani Manispaa ya Ilala kusimamia na kupitisha shuguli za Miradi ya maendeleo bila kukwamisha wala kuichelewesha kwa kuendekeza mivutano kwani lengo la miradi Ni kutatua kero zinazowakabili wananchi.

Rc Makonda ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na kudai kuwa kumekuwa naucheleweshaji wa miradi kwa maslahi  binafsi na kuelekeza ofisi ya Katibu tawala mkoa kuhamisha watumishi na wakuu wa Idara wanao kwamisha kazi hizo.

Aidha amepongeza kwa kuanza kwa ujenzi wa soko la Kisutu na machinjio ya kisasa ya Vingunguti baada ya kukwama.

"Miradi hii ya kimkakati tumepewa fedha, naomba tuisimamieipasavyo ili tutatue kero zilizopo Katika halmashauri zetu" Amesema Makonda.

Amewataka  madiwani hao kuacha mivutano  na kuongeza bidii ya kusimamia miradi ilikuokoa fedha za walipakodi na kumuagiza Mkurugezi kufanya maamuzi ya kumpa kazi ya kujenga mifereji ya Maji ya mvua Mkandarasi ambaye atafanya ujenzi haraka iwezekanavyo.

"Jambo lingine ambalo linatukwamisha pia ni kutoaminiana naomba tuaminiane ili mambo yaende naomba kama mtakwama nipo muda wote nipigieni  simu wala haihitaji kutuma barua"Amesema.

Aidha amesema wakuu wa Idara wanaokwamisha maendeleo Hadi kufika May 30, mwaka huu,wawe wamamishwa ili kuepusha migongano na mivutano inayotokea hivyo amewataka kuelekeza nguvu kwa Pamoja ili kuhakikisha miradi haichelewi Tena.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages