Dar es Salaam, Aprili 17, 2019 - Sasa wasafiri wanaotumia mfumo wa Uber wanaweza kutoa tip kwa madereva baada ya safari - hii inatokana na kipengele kipya ambacho kampuni ya Uber imetangaza leo. Kipengele cha kutoa tip kinawapa wasafiri wanaotumia Uber fursa ya kuonyesha shukrani zao kwa huduma nzuri wanayopata kutoka kwa madereva-washirika wa Uber. Pesa zote zitakazotolewa kama tip zitamwendea dereva husika moja kwa moja na hakuna ada yoyote ya huduma itakayotozwa pesa hizi.
Meneja wa Uber Kusini mwa Jangwa la Sahara Alon Lits, anaelezea; “Kuendesha gari ni zaidi ya kumtoa msafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine. Madereva- washirika wanaotumia mfumo wetu wanajituma kila siku, ili kuhakikisha kwamba wanawarahisishia wasafiri wetu shughuli zao za kila siku - kuwafikisha kwenye mikutano muhimu ya kikazi, kuwapeleka nyumbani baada ya shamrashamra za mitoko ya jioni - wanafanya kila aina ya safari. Hii ndiyo maana tumeweka mkazo na tunafanya juhudi endelevu katika kuimarisha huduma zetu.”
“Ujio wa kipengele hiki unatokana na maoni tuliyopokea kutoka kwa madereva- washirika kupitia vikao mbalimbali ambavyo tumekuwa navyo ikiwa ni mkakati wa kuboresha na kuimarisha huduma zetu. Kupitia kipengele hiki, Uber inatoa njia ambayo madereva-washirika, wanaojituma kwa kutoa huduma nzuri kwa wasafiri, watatambuliwa na kutuzwa kwa kazi nzuri wanayoifanya. Madereva kama hawa ni wale husubiria hadi wahakikishe mteja ameingia nyumbani kabla waondoke.” amehitimisha Bw. Lits.
Msafiri kutumia kipengele hiki ni hiari kwa 100% na wasafiri watapewa kiasi fulani ambacho watachagua tip ambayo wangependa kumpa dereva. Kipengele hiiki kitakuwa sehemu ya chini ya tathmini na pongezi ya app.
Malipo yote ya tip yatakatwa kwenye kadi ya benki ya msafiri iliyosajiliwa kwenye mfumo wa Uber, kwa wasafiri wanaolipa kwa njia ya keshi wako huru kumpa dereva tip moja kwa moja.
Hivi ndivyo inavyofanya kazi:
· Jinsi ya kumpa dereva tip
· Pakua toleo jipya la app.
· Mwishoni mwa safari yako, ongeza tip
baada ya kutathmini safari yako.
· Chagua mojawapo kati ya kiasi
kilichowekwa au uweke kiasi unachotaka.
· Bonyeza Nimemaliza ili utume tip yako.
· Pesa zote za tip zitatumwa kwa dereva
moja kwa moja, Uber haitatoza ada
· yoyote ya huduma kwenye tip.
No comments:
Post a Comment