Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya
DCB , James Ngaluko (wa tatu kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam leo,
wakati wa uzinduzi wa akaunti mpya ya muda maalum ijulikanayo kwa jina la ‘DCB
Lamba Kwanza’ inayomuwezesha mteja kupata riba ya hadi asilimia 14 papo hapo
mara baada ya kuwekeza. Wengine kutoka kushoto ni; Meneja wa DCB Tawi la
Temeke, Anna Kasyupa, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa,
Meneja wa Akaunti za Kidigitali, Fredrick Mwakitwange na Meneja wa Tawi la DCB
Magomeni, Fortunata Benedict.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya
Biashara ya DCB, Rahma Ngassa (wa pili kushoto), akizungumza jijini Dar es
Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa akaunti mpya ya muda maalum ijulikanayo kwa
jina la ‘DCB Lamba Kwanza’ inayomuwezesha mteja kupata riba ya hadi asilimia 14
papo hapo mara baada ya kuwekeza. Wengine kutoka kushoto ni; Meneja wa DCB Tawi
la Temeke, Anna Kasyupa, Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko, Meneja wa
Akaunti za Kidigitali, Fredrick Mwakitwange na Meneja wa Tawi la DCB Magomeni,
Fortunata Benedict.
Benki ya biashara ya DCB imezindua bidhaa
maalumu kwa ajili ya wateja wa akaunti ya muda maalum (Fixed Deposit)
ijulikanayo kama ‘DCB LAMBA KWANZA’.
Bidhaa hii mpya itamuwezesha mteja
wa DCB kuwekeza hadi miaka miwili na kupata riba ya hadi asilimia 14% ya amana
atakayo wekeza na riba ya mwezi italipwa
papo hapo pindi anapofungua akaunti.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa bidhaa hii jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa
Biashara, James Ngaluko alisema Akaunti hii
itamuwezesha mteja wetu kupata riba kila mwezi hivyo kufanya wateja wa DCB kufurahia maisha kwani kila mwezi ni mwezi wa
faida.
‘Riba inalipwa mwanzo wa mwezi kila mwezi, malipo ya riba ni rafiki
mteja anaweza kuwekeza kuanzia miezi mitatu (3) mpaka miaka miwili (2). Ni
matumaini yetu wateja wetu watachangamkia fursa hii na watafurahia akaunti hii kwani tumeboresha maisha na uchumi’.
Alisema Lengo kubwa la kuanzishwa
kwa akaunti hii ni kuwapa fursa wateja wa DCB kuweza kuwekeza kwa faida na
manufaa. Wateja na wasio wateja wa DCB wanaweza sasa kufungua akaunti hii ya DCB Lamba Kwanza na kuweza kuwekeza.
‘Tumekuja
na jina hili la ‘DCB Lamba Kwanza’
kama lilivo neno lenyewe, mteja wetu ataweza kulamba riba ya mwezi papo hapo
pindi atakapofungua akaunti’ aliongeza mkurugenzi wa biashara.
Pamoja
na hayo Bwana Ngaluko aliongeza kuwa akaunti ya DCB lamba kwanza HAINA STRESS kwani itamuwezesha mteja
kupata kipato kikubwa kila mwezi kwa kipindi kirefu, hivo kuitofautisha na
akaunti nyingine kama hizi…..’ukiwa na
akaunti ya DCB lamba kwanza kila mwezi ni mwezi wa mshahara’.
Mteja
anaweza kufungua akaunti katika tawi lolote la DCB ama kupitia huduma za
kidigitali kwa kupiga *150*85# huku mteja akihakikishiwa usalama wa pesa zake wakati huohuo hakuna makato ya akaunti ya
kila mwezi na hakuna gharama ya kufungua akaunti.
Ikumbukwe
kuwa Benki ya Biashara ya DCB
ilianzishwa mwaka 2002 ikiwa kama Benki ya Jumuiya ya Wananchi “community bank”
na Manispaa za Jiji la Dar es Salaam kufuatia kilio cha wakazi wengi wa Jiji
kutokuwa na njia rahisi ya kupata mitaji midogo midogo ya biashara. Benki ya DCB
imekuwa ni benki ya kwanza kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa mwaka 2008, na
imeweza kukuza mtandao wake wa matawi kufikia matawi nane likiwepo tawi la
Dodoma, na inatarajia kuongeza matawi mengine mikoani katika miaka ya mbeleni.
Uboreshaji huduma na mahusiano ya wateja umekuwa
ndio kigezo kikuu katika kuongeza amana nafuu na za muda mrefu hasa kutoka kwa
wanahisa waanzilishi na mashirika mbalimbali yaliyoendelea kuwekeza na benki ya
DCB.
Huduma za kidigitali zimekuwa chachu ya kuongeza
ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji na gharama za riba. Akaunti hizi
zinajumuisha akaunti ya kidijiti (DCB Digital Account), DCB Kibubu Digital
Account, DCB FDR Digital account. Akaunti hizi zinamuwezesha mteja kufungua
akaunti na kufanya miamala yote ya kibenki, Kutunza pesa na kuwekeza kwa
kutumia simu yake ya mkononi.
Idadi ya wateja imeongezeka kutoka 144,475 mwaka 2017 kufikia 175,204 mwaka 2018 na hivyo kuchangia
ongezeko kubwa la miamala ya kibenki.
1. Benki ya DCB ndio benki ya kwanza
kuorodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam.
2. Benki ya DCB ndio benki pekee
iliyokua kutoka benki ya wananchi/jamii (community bank) na kufanikiwa kuwa
benki ya biashara (commercial bank).
3. Benki ya DCB imefanikiwa kukuza
mtandao wa matawi yake kufikia manane huku ikifungua tawi Dodoma na inaendelea
na mchakato kufungua matawi na vituo vya huduma (service centers) katika mikoa
mingine.
4. Benki ya DCB imefungua mtandao wa
mawakala na huduma za kijiditali hadi kufikia 1000.
No comments:
Post a Comment