TANZANIA YANG’ARA KATIKA MAONYESHO YA UTALII SEOUL, KOREA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, June 20, 2019

TANZANIA YANG’ARA KATIKA MAONYESHO YA UTALII SEOUL, KOREA

Ubalozi wa Tanzania Seoul, kwa kushirikiana na wadau wa Utalii kutoka sekta binafsi wameshiriki katika maonyesho makubwa ya Kimataifa ya “Seoul International Tourism Industry Fair” yaliyofanyika jijini Seoul kuanzia Juni 6-9, 2019 na kuandaliwa na Korea World Travel Fair (KOTFA) kwa kushirikiana na Seoul International Travel Mart (Seoul Metropolitan City).
Maonyesho hayo makubwa na ya aina yake yalijumuisha wadau kutoka nchi mbalimbali za Asia, Ulaya, America, Africa na Middle East wakiwemo:  Tour Operators, Travel Fairs, wamiliki wa Hoteli na Migahawa (Restaurants), Media, na wamiliki wa vyombo vya usafiri (Ndege, Cruise ships).
Tanzania iliwakilishwa na Ubalozi wa Tanzania Korea Kusini, Kampuni ya Utalii Eastenders, Zara Tours, Travel Booking Guide kwa kupitia Mwakilishi wake aliye Korea, Ms. Han Bitnarae, na SAFANTA Tours & Travel ya Zanzibar.
Kwa ujumla maonyesho hayo yalifana sana kwa Makampuni hayo kupata wenzao wa kushirikiana nao kibiashara kupitia B2B, kubadilishana uzoefu, kupata wateja wenye nia ya kwenda kutembelea Tanzania, na kwa kiwango kikubwa kuitangaza Tanzania katika jamii ya Wakorea na Mataifa mengine, ili wafahamu vivutio vilivyopo Tanzania, hali ya Usalama na Utulivu, na uwepo wa huduma nzuri za Malazi, Vyakula na Usafiri.   
Balozi wa Tanzania Korea Kusini, Mhe. Balozi Matilda Swilla Masuka (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Tanzania katika maonyesho hayo, pamoja na wageni waliotembelea banda la Tanzania.
Picha ya pamoja kati ya washiriki wa Maonyesho hayo ya Utalii, Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Seoul, na Watanzania waishio Korea Kusini (Diaspora) ambao walikuja kuunga mkono juhudi hizo za kuitangaza Tanzania.
Timu ya Kampuni ya Eastenders Tours & Safari ikiongozwa na Mkurugenzi wake Bi. Masha H. Kimaro wakiwa katika mkutano wa B2B (Travel Mart) na Makampuni ya Kikorea kubadilishana uzoefu na kujadiliana maeneo ya ushirikiano wa kibiashara. Makampuni kadhaa yameonyesha nia, na wamefikia hatua nzuri ya makubaliano.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages