Na Mwandishi wetu
Taasisi isiyo ya
kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation, imezindua ripoti yake ya mchango wa
maendeleo ya jamii kwa miaka mitatu iliyopita (2014-2017) pamoja na mkakati mpya
wa miaka mitatu 2019-2021 unaolenga kuchochea elimu jumuishi, ukuaji wa sekta
ya kilimo, kuboresha mazingiza na ujumuishwaji wa watu kwenye mifumo rasmi ya
kifedha.
Uzinduzi huu umefanyika
katika tukio lililopewa jina la "Alama za upendo wa Vodacom" na kuhudhuriwa
na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -
Afya), Mhe. Josephat Kandege, maafisa kutoka washirika wa maendeleo na wadau wa
kitaifa na kimataifa jijini Dar es Salaam.
Taasisi ya Vodacom
Foundation imewekeza zaidi ya TZS bilioni 11 katika miradi ya jamii ambayo imeinua
na kuboresha maisha ya watu takribani milioni 3 nchini, kupitia miradi
mbalimbali hususani afya ya uzazi, elimu na huduma jumuishi za kifedha.
Mgeni rasmi katika
uzinduzi huo, Mheshimiwa Kandege alipongeza jitihada za Vodacom Tanzania Foundation
katika kusaidia jamii na kusisitiza ushirikiano kati ya wadau mbalimbali.
"Nawapongeza sana Vodacom kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha
maisha ya Watanzania na hasa katika sekta ya afya ya uzazi, elimu na uwezeshaji
wa kiuchumi. Kuendeleza Tanzania ni jukumu letu sote hivyo basi ni muhimu sana tuungane
pamoja kutimiza azma hii ya taifa letu. Natumai kwamba ripoti hii itatuhamasisha
sote kuchangia Nguvu katika kuboresha maisha ya watanzania" aliongeza
Mheshimiwa Kandege.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa
Vodacom Tanzania, Bw. Hisham Hendi akizungumza juu ya mkakati huo mpya wa Taasisi
hiyo alisema, "Mkakati wetu wa 2019-2021 umezingatia mipango ya maendeleo
ya nchi (Tanzania) na malengo endelevu ya maendeleo (SDGs) huku tukilenga
kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha, ubora wa elimu na kuchochea
mabadiliko katika sekta ya kilimo. Kama mtandao wa simu unaoongoza nchini, tuna
nafasi ya pekee kuchangia maendeleo ya jamii na ya kiuchumi nchini kwa kupitia matumizi
ya teknolojia ya simu."
Mkurugenzi huyo aliongeza
kuwa kampuni za simu zina fursa kubwa na wajibu wa kutumia teknolojia na
uvumbuzi wa kidijitali kukuza uchumi wa nchi kwa kuongeza ufanisi wa watu. Kampuni
ya Vodacom imekuwa ikifanya hivyo tangu mwaka 2000.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, Bi. Rosalynn Mworia, alisisitiza
mashirika kuwekeza katika miradi inayolenga kutatua changamoto mbalimbali za kijamii.
"Tumeshirikisha wadau mbalimbali katika uzinduzi wa ripoti hii ili kuwahamasisha
kuwekeza katika miradi ya kuboresha jamii na kuchochea ushirikiano zaidi baina
yetu na wao ili kufikia lengo la kuwa taifa lenye maendeleo jumuishi.”
aliongeza Rosalynn.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006, Taasisi ya Vodacom Tanzania
Foundation imekuwa ikishirikiana na taasisi mbalimbali, imechangia vilivyo katika
kuboresha maisha ya Watanzania kupunguza umasikini, kuboresha elimu, kuwezesha
Wanawake na Wasichana, pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya ya
uzazi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa Afya Mh. Josephat Kandege, (kulia), akisalimiana na
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Hashim Hende, wakati wa Uzinduzi wa ripoti ya
Maendeleo ya jamiI na mkakati mpya wa kuchochea ukuaji jumuishi uliopewa jina
la Alama za upendo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni
Mwenyekiti wa Bodi TCRA, Dk John Killimbe.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa Afya Mh. Josephat kandege (watatu kushoto), akimsikiliza
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Hashim Hende (kulia), wakati wa Uzinduzi wa ripoti
ya Maendeleo ya jamiI na mkakati mpya wa kuchochea ukuaji jumuishi uliopewa
jina la Alama za upendo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wengine (kushoto),
ni Mwenyekiti wa Bodi TCRA, Dk John Killimbe pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya
Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa Afya Mh. Josephat kandege (watatu kushoto) akimsikiliza
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia wakati
akimuonesha picha maalum zilizoandaliwa na Vodacom wakati wa Uzinduzi wa ripoti
ya Maendeleo ya jamiI na mkakati mpya wa kuchochea ukuaji jumuishi uliopewa
jina la Alama za upendo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kushoto kwa Waziri
ni Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Hashim Hende pamoja na Mwenyekiti wa Bodi TCRA,
Dk John Killimbe.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Hashim Hende akipiga
picha ya pamoja na wageni waalikwa.
No comments:
Post a Comment