Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii profesa Adolf Mkenda (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN unaotolewa na benki ya CRDB jijni Arusha.
Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii profesa Adolf Mkenda (kulia) akiwa katika moja ya gari katika halfa ya uzinduzi wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN unaotolewa na benki ya CRDB jijni Arusha.
Moja ya gari katika halfa ya uzinduzi wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN unaotolewa na benki ya CRDB jijni Arusha.
Mwenyekiti wa bodi ya utalii Tanzania jaji mstaafu Thomas Mihayo akimkabidhi ufunguo wa gari jipya mmoja wa wadau aliyenufaika na mkopo wa benk ya CRDB wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN uliozinduliwa jana jijini Arusha.
Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii profesa Adolf Mkenda akimkabidhi ufunguo wa gari mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Samless adventures Sam Manonga baada ya kupata mkopo kutoka benki ya CRDB katika halfa ya uzinduzi wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN unaotolewa na benki ya CRDB.
Mwenyekiti wa bodi ya utalii Tanzania jaji mstaafu Thomas Mihayo akimkabidhi ufunguo wa gari jipya mkurugenzi wa kampuni ya Nature responsible safari Bi Francisca Masika ambae ni mwanamke pekee aliyenufaika na mkopo wa benk ya CRDB wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN uliozinduliwa jana jijini Arusha.
Mwenyekiti wa bodi ya utalii Tanzania jaji mstaafu Thomas Mihayo akimkabidhi ufunguo wa gari jipya mkurugenzi wa kampuni ya Nature responsible safari Bi Francisca Masika ambae ni mwanamke pekee aliyenufaika na mkopo wa benk ya CRDB wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN uliozinduliwa jana jijini Arusha.
Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii Profesa Adolf Mkenda akimkabidhi ufunguo wa gari jipya mkurugenzi wa kampuni ya Excelent guides Diason baada ya kupata mkopo wa CRDB wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN uliozinduliwa jana jijini Arusha.
Mmoja wa wadau akipongezwa kwa mkopo wa benk ya CRDB wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN uliozinduliwa jana jijini Arusha.
Wafanyakazi wa benk ya CRDB wakifurahia mapokeo ya zao jipya la SAFARI CAR LOAN uliozinduliwa jana jijini Arusha.
Katika
kuunga mkono jitihada za serikali za kukuza sekta ya utalii nchini benki ya
CRDB imezindua zao jipya la kibiashara liitwalo “SAFARI CAR LOAN”zao ambalo
lina lengo la kuwawezesha wajasiriamali waliopo katika sekta hiyo
kufanya biashara yao kwa ufanisi kwa kuwapatia mikopo ya magari mapya
ya utalii kwa riba nafuu.
Mkopo huo
wenye riba ya asilimia 10 unatolewa na benki ya CRDB ambayo imeingia mkataba na
kampuni ya utengenezaji magari maalum ya utalii ya Hanspaul ya jijini Arusha
ambayo gari jipya hugharimu kiasi cha dola elfu sabini na tano hadi laki moja
ambayo mkopaji atarejesha mkopo ndani ya miaka mitano.
Afisa biashara
Mkuu wa Benki ya CRDB ,Dakta Joseph Witts akizungumza hafla maalum ya uzinduzi
wa zao hilo la Safari Car Loan jijini Arusha iliyoenda sambamba na
kongamano la utalii liloshirikisha a wafanyabiashara kutoka Hongkong China
,Tanzania na taasisi za serikali zinazojihusisha na uwekezaji dakta Witts
alisema lengo la kuanzisha zao hilo ni kutatua changamoto ya usafiri usafiri
katika sekta hiyo.
“CRDB
tumekuja kutatua changamoto kubwa ambayo wafanyabiashara wamekuwa wakikumbana
nayo kutokana na ukosefu wa mitaji ya kuweza kununua magari ya kusafirishia
watalii tukijua kwamba utalii unachangia sehemu kubwa katika pato la taifa” alisema
Witts.
Kwa upande
wake Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii profesa Adolf Mkenda aliipongeza
benki ya CRDB kwa uvumbuzi wa zao jipya la kibenki ambalo
litasaidia wajasiriamali kuweza kujipatia magari ya kusafirisha watalii kwa
uhakika Zaidi.
“Uvumbuzi
huu wa zao jipya la biashara la kibenk linasaidia wajasiriamali kuweza
kujipatia magari ya kubeba watalii, huu ni ubunifu mzuri utasaidia vijana wetu
ambao hawana mitaji mingi kuweza kujiingiza kwenye shughuli hizi hususani wakati
huu ambao serikali ikiiendelea kuongeza vivutio vya utalii nchi” alisema Mkenda.
Kwa pande
wao baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo bi Fransisca Masika mkurugenzi wa kampuni
ya Nature Rensiposible Safari na S.M. Mwanonga mkurugenzi wa kampuni ya SAMLESS
Adventures wameishukuru CRDB kwa mkopo huo ambao walisema utaboresha biashara
yao.
No comments:
Post a Comment