Mkurugenzi wa Mahusiano wa Benki ya CRDB, Tully Ester Mwambapa akizungumza jambo wakati alipokuwa akiongoza Kongamano la uwezeshaji kibiashara lililoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wanaohusika na utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo nchini, lililofanyika leo kwenye ukumbu wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Afisa
Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akizungumza katika
Kongamano la uwezeshaji kibiashara lililoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya
Wakandarasi na wadau mbalimbali wanaohusika na utekelezaji wa ujenzi wa miradi
mikubwa ya maendeleo nchini, lililofanyika leo kwenye ukumbu wa Hoteli ya
Serena, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Wateja wa Kati na Wadogo wa Benki ya CRDB, Boma Raballah akizungumza katika
Kongamano la uwezeshaji kibiashara lililoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya
Wakandarasi na wadau mbalimbali wanaohusika na utekelezaji wa ujenzi wa miradi
mikubwa ya maendeleo nchini, lililofanyika leo kwenye ukumbu wa Hoteli ya
Serena, jijini Dar es salaam.
Benki ya CRDB imeandaa kongamano maalum la uwezeshaji kibiashara
kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wa ujenzi wa miradi ya maendeleo
nchini ikiwamo ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge Railway) na mradi wa
uzalishaji umeme wa bonde la mto Rufiji (Rufiji Hydropower Project).
Akizungumza wakati wa kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na
makampuni zaidi ya 400 ya ukandarasi na watoa huduma mbalimbali, Afisa Biashara
Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts alisema kongamano hilo limelenga
katika kuwajengea uwezo wakandarasi nchini ili kuwasaidia kutekeleza miradi yao
kwa ufanisi zaidi.
“Benki yetu ya CRDB imeweka mikakati mikubwa katika
kuhakikisha tunaisaidia Serikali yetu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali
ya Maendeleo, tulianza kwa kutoa mikopo na dhamana katika miradi mbalimbali
ikiwamo mradi wa reli ya kisasa ya SGR na mradi wa umeme wa maji wa Rufiji
(RHPP). Sasa hivi tumejipanga kuongeza wigo wetu katika kuwasaidia wakandarasi
na watoa huduma katika miradi hii, kwani hawa ndio watekelezaji wenyewe,”
alisema Dkt.Witts.
Dokta Witts alisema benki hiyo kupitia kauli mbiu yake ya
“Tupo Tayari” imejipanga vilivyo kuwahudumia Wakandarasi hao nchini huku
akitaja baadhi ya huduma ambazo benki hiyo inazitoa kwa ajili ya wateja kupitia
idara yake ya wateja wakubwa.
“Benki yetu sasa hivi inatoa huduma ya dhamana kwa
wakandarasi au wateja ambao wanatafuta kazi ijulikanayo kama ‘Bid Guarantee’
hii inatuwezesha kumjengea mkandarasi uwezo wa kupata kazi, lakini vilevile
tunatoa dhamana za utekelezaji wa miradi ‘Performance Guarantee’ na dhamana za
malipo ya awali ‘Advance Payment Guarantee’,” alisema Dkt. Witts.
Dkt. Witts alisema Benki hiyo imeboresha taratibu zake za
utoaji mikopo akiwataka wakandarasi hao kujitokeza kwa wingi kuomba mikopo,
pamoja na kujiunga na huduma za bima ili kujikinga na majanga yanayoweza
kutokea. “Benki ya CRDB ni Benki yenu, na sisi tupo hapa kuwahudumia
niwahakikishie tu sisi Tupo Tayari kuwahudumia,” alihitimisha Dkt. Witts.
Kwa upande wake Msajili Mkuu wa Wakandarasi nchini (CRB),
Rhoben Nkori aliipongeza Benki ya CRDB kuwa mstari wa mbele kuwezesha
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini huku akiwataka wakandarasi
wote kuchangamkia fursa hiyo inayotolewa na Benki ya CRDB katika kukuza na kuboresha
utendaji wa kazi zao.
Wakandarasi na wadau mbalimbali waliohudhuria kongamano hilo
waliipongeza Benki ya CRDB kwa hatua hiyo ya kuwakutanisha wadau wa sekta ya
ujenzi nchini huku wakieleza fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB zitakwenda
kuleta sura mpya katika utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu nchini.
No comments:
Post a Comment