KATIBU UVCCM BAGAMOYO AWATAKA VIJANA KUTOKUWA CHANZO CHA MPASUKO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, October 2, 2019

KATIBU UVCCM BAGAMOYO AWATAKA VIJANA KUTOKUWA CHANZO CHA MPASUKO


Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Bagamoyo ndugu Omary Ally, (aliyesimama), akizunguimza wakati wa hafla fupi yakuwapongeza vijana wa kata ya Mapinga waliohitimu Mafunzo yaujasiriamali katika kambi maalum iliyodumu kwa siku kumi  kwa vijana wa wilayani humo hafla hiyo imefanyika Bagamoyo  hivi karibuni.

Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Bagamoyo ndugu Omary Ally amewasihi Vijana kuwa wavumilivu hasa Katika kipindi hiki cha Uchaguzi ili kuepusha Migongano ndani ya Chama yenye kuleta Mipasuko ambayo Miaka yote ndio imewanufaisha Vyama vya upinzani kwenye Chaguzi.

Katibu huyo ameyasema hayo wakati alipoalikwa kuwa Mgeni wa Rasmi kwenye  hafla ya kuwapongeza Vijana wa kata ya Mapinga waliohitim Mafunzo ya Ujasiriamali Katika Kambi maalum ya Vijana wilayani humo  iliyofanyika kwa siku 10.

Pamoja na hayo Ndugu Omary Aliwataka Vijana hao kutembea Kifua mbele kwakua Serikali ya awamu ya Tano imefanya Mengi Makubwa katika kuketa maendeleo nchini na yote yanaonekana hivyo kila wanapokaa basi wayaseme mafanikio hayo.


"Ndugu zangu Nchi yetu kwa Sasa inaongoza miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara Katika kupambana na Umasikini na jitihada hizi zinachochewa sana na Kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli hivyo tuendelee kumuombea Rais wetu Kwani Sasa Taifa letu limepiga hatua kubwa kupitia yeye " alisema Kaimu Katibu huyo.

Katika Hafla hiyo Diwani wa Kata ya Mapinga ndugu Mbonde naye alipata Nafasi ya kueleza Utekelezaji wa ilani ya ccm Katika kipindi cha miaka minne  ambapo ameishukuru serikali kwa kufanikisha Ujenzi wa Zahanati pamoja na Shule mbili za Msingi pamoja na Shule ya Sekondari Kata ya Mapinga.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages