Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mhe. Paul Makonda amewataka Wakala wa Majengo Tanzania TBA kuhakikisha ujenzi
wa Jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo unakamilika na kuanza kutumika
kabla ya Disemba 30 Mwaka huu likiwa Viwango na Ubora unaotakiwa.
RC Makonda amechukizwa
kuona mkataba wa ujenzi huo umesainiwa tokea Disemba 13 mwaka jana na kazi
inatakiwa kukamilika Disemba 13 mwaka huu lakini hadi sasa ujenzi umefikia 35%
huku muda wa mkandarasi kuwa site ukiwa mkubwa kuliko kazi aliyoifanya.
Kilichomkwaza zaidi RC
Makonda ni kubaini kuwa ujenzi ulisimama kwa zaidi ya Miezi miwili kwa kigezo
cha Manispaa kuchelewa kutoa fedha huku muhusika akikaa kimya pasipo kutoa
taarifa kwenye ngazi ya Mkoa ili mkoa uweze kuingilia kati fedha itoke kwa
wakati.
Aidha RC Makonda
amefanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la Kisasa la Juu
(Interchange) Ubungo ambapo ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo na kumuelekeza
mkandarasi kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.
Pamoja na hayo RC
Makonda pia amefanya ziara ya Ukaguzi wa Maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya
njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha na kueleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi
huo.
Katika ziara hiyo RC
Makonda ametembelea Ujenzi wa Kituo cha Afya Kimara na kumuelekeza Katibu
tawala wa Mkoa huo kutuma timu ya kufuatilia upya ujenzi wa Jengo la gorofa
katika kituo hicho linalogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 1.2 baada ya
kubaini gharama za ujenzi ni kubwa kuliko idadi ya majengo wakati Wilaya ya
Kigamboni imetumia Bilioni 1.5 kujenga majengo saba ya kisasa.
No comments:
Post a Comment