CHAMA CHA CUF CHAUNGA MKONO MAAMUZI YA SERIKALI KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA CORONA (COVID-19) NCHINI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, April 16, 2020

CHAMA CHA CUF CHAUNGA MKONO MAAMUZI YA SERIKALI KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA CORONA (COVID-19) NCHINI


CUF- Chama Cha Wananchi kinapenda kuunga mkono Maamuzi ya Serikali ya kutangaza kuendelea kufungwa kwa Shule na Vyuo vya Elimu ya Juu pamoja na kuendelea kusimamisha mikusanyiko ya shughuli za Michezo katika kupambana na kuenea kwa  Maambukizi ya COVID-19.  CUF-Chama Cha Wananchi kinaunga mkono pia Uamuzi wa kufuta Sherehe za Muungano na Mei Mosi kwa mwaka huu na pia Maamuzi ya kuelekeza Shilingi Milioni 500 zilizopangwa zitumike kwenye Sherehe za Muungano, kwenye Mfuko wa Kupambana na COVID-19 wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Aidha CUF-Chama Cha Wananchi kinaungana na Serikali katika kutoa Msisitizo kwa wadau katika kuchangia harakati za Mapambano dhidi ya Corona (COVID-19). Kwa hakika Mapambano haya ni yetu sote na hayana Itikadi iwe ya chama au dini.

Pamoja na kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kutoa Elimu juu ya Ubaya wa Mikusanyiko isiyolazimu, CUF-Chama Cha Wananchi kimepata taarifa juu ya Uwepo wa Vyuo vya Umma vilivyoamua kuendeleza Masomo kwa Njia ya Mitandao (Online Sessions). Ukweli utokanao na uzoefu unathibitisha kwamba zaidi ya nusu ya wanaosoma kwa njia za mitandao hapa nchini hawana Uwezo wa kupata huduma hiyo wakiwa majumbani mwao, bali hutegemea huduma za internet cafe.

Kuendeleza Mafunzo haya (Online Sessions) ni Sawa na kuhamishia hii mikusanyiko kwenye hizi Internet cafes. Hivyo CUF-Chama Cha Wananchi kinatoa wito kwa Serikali kuviagiza Vyuo Vikuu nchini kusimamisha kabisa Programu Rasmi za kimasomo zinazoweza kuwalazimu watoto wa walala hoi kutoka majumbani mwao ili wapate huduma za Mtandao kwenye vibanda vya biashara na kuzorotesha Mapambano dhidi ya kuenea kwa COVID-19 au kuwanyima haki ya Kielimu watoto hawa.

Tunashauri Ratiba zote zisubiri tushinde Mapambano haya dhidi ya janga hili la Ulimwengu.

CUF- Chama Cha Wananchi kinaendelea kutoa Wito kwa Viongozi wa Dini zote na Wananchi kwa Ujumla kutopuuzia Maradhi haya Bali sote tupambane kulitokomeza janga hili kwa kuzingatia Maelekezo ya Wataalam sanjari na kumtegemea Mwenyezi Mungu.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages