MANISPAA YA TEMEKE YAPOKEA VIFAA VYA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, April 16, 2020

MANISPAA YA TEMEKE YAPOKEA VIFAA VYA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA

Meya wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Alhaj Abdallah Chaurembo(kulia) akikabidhi Sanitizer kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mbagala leo.Msaada huo umetolewa na Kampuni ya General Petroleum.
Meya wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Alhaj Abdallah Chaurembo (wa pili kulia)akipokea msaada wa barakoa, glovu pamoja na Sanitizer  kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya General Petroleum Ltd Hayatulah Khan (wa tatu kushoto) kwa ajili ya kugawa kwa watumishi na watendaji wa manispaa hiyo. Msaada huo umekabidhiwa leo ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kukabiliana na ugonjwa Covid-19  unaosababishwa na virusi vya Corona.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya General Petroleum Ltd Hayatulah Khan (aliyesimama) akizungumza mbele ya watendaji na watumishi wa manispaa ya Temeke jijiini Dar es Salaam kabla ya kukabidhi msaada wa Sanitizer, Barakoa pamoja na glovu ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19. Aliyekaa ni Meya wa Manispaa ya Temeke Alhaj Abdallah Chaurembo.
Meya wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Alhaj Abdallah Chaurembo akizungumza leo kwenye ukumbi wa manispaa hiyo kabla ya kupokea msaada wa barakoa, sanitizer na glovu kutoka Kampuni ya  General Petroleum(GP) kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa Covid-19.
Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaama wakiwa ukumbini wakati wa upokeaji wa msaada wa vifaa vya Barakoa, Sanitizer na Glovu ambazo zimetolewa na Kampuni ya  General Petroleum.
Meya wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Alhaj Abdallah Chaurembo (kushoto) akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Gwamaka Mwabulambo (kulia) baada ya kupokea msaada wa Sanitizer, Barakoa na Glovu ambazo ni msaada kutoka Kampuni ya General Petroleum kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 unaosabishwa na virusi vya Corona.
Baadhi ya maofisa kutoka Kampuni ya General Petroleum wakiwa pamoja na Meya wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia), wakiwa na Sanitizer kabla ya kuanza kwa kugawa kwa watendaji, madiwani na watumishi wa manispaa hiyo.
Sehemu ya maofisa wa Kampuni ya General Petroleum (waliovaa fulana) wakiwa katika ukumbi wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam .Wengine ni viongozi wa manispaa ya Temeke wakifuatilia maelekezo ya kutumia vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa virusi vya Corona.
Baadhi ya madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam wakipaka Sanitizer baada ya kupewa msaada huo kutoka Kampuni General Petroleum.
Meya wa Manispaa ya Temeke Alhaj Abdallah Chaurembo(kulia) akikabidhi kasha lenye Sanitizer kwa Ofisa Ugawi katika Hospitali ya Temeke Khalid Mtaraziki. Wengine ni maofisa wa Kampuni ya General Petroleum.

Diwani wa Kata ya Kilungule Said Fella akiwa na baadhi ya viongozi wa manispaa ya Temeke wakati wa utolewaji wa msaada wa Sanitizer, glovu na barakoa.

KAMPUNI ya General Petroleum imekabidhi msaada wa Sanitizer, barakoa na glovu kwa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona huku Meya wa Manispaa hiyo Alhaj Abdallah Chaurembo akisisitiza umuhimu wa wananchi kufuata maelekezo ya watalaam wa afya.

Akizungumza leo wakati wa kupokea vifaa hivyo Meya Chaurembo amesema Wilaya ya Temeke imekuwa ikichukua tahadhari katika kukabiliana na ugonjwa huo kwa kuwakumbusha wananchi kuendelea kufuata maelekezo ya watalaam wa afya na kwamba msaada ambao wameupata kutoka kwenye kampuni hiyo umekuja wakati muafaka na kwamba watahakikisha unawafikia wananchi mbali ya viogozi na watendaji.

"Vifaa hivi vitasabazwa kwenye Kata zote za Manispaa hii, niwaombe wananchi kuvitumia kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya, lakini pia tuendelee kuchukua tahadhari kama ambavyo Serikali inatuelekeza," amesema Alhaj Chaurembo.

Aidha,amesema vifaa hivyo vitapelekwa pia kwenye hospital ya rufaa ya Mkoa ya Temeke pamoja na Hospital ya Wilaya ya Mbagala Zakheem.Ambapo  baada ya kutoka katika manispaa hiyo walikwenda kukabidhi msaada huo kwa hospitali hizo. Pia amekabidhi kwa watendaji na madiwani wa kata zote zilizopo ndani ya manispaa hiyo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dk. Gwamaka Mwabulambo amesema wananchi wanatakiwa kufahamu kuwa ugonjwa huo hauna tiba na jambo muhimu ni kuchukua tahadhari. "Tuendelee kuchukua tahadhari Kwa kuepuka msongamano na kushikana mikono."

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Hayatulah Khan amesema baada ya kuona jitihada ambazo zinafanywa na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo, wameona wanayo nafasi ya wao kusaidia vifaa vya kukabiliana na Corona na hivyo wamekabidhi msaada wao kwa manispaa ya Temeke. "Tupo tayari kuendelea kutoa msaada zaidi katika kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19."

Wakati huo huo Ofisa Rasilimali watu wa General Petroleum, Aboubakar Kondo, amefafanua kampuni yao inaguswa na tatizo lililoikumba Tanzania na Dunia kwa ujumla la virusi vya Corona, hivyo  wameona ni vema wakasaidia vifaa hivyo kwa kupeleka manispaa ya Temeke, Hospitali ya Mkoa wa Temeke pamoja na Hospitali ya Mbagala na kwamba wataendelea kugawa na kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages